Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za wachezaji imetoa siku tatu
kuanzia jana Septemba 24, 2016 kwa
viongozi wa klabu za Simba SC na Young Africans SC kukaa chini na kumaliza suala la usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kwa njia ya mazungumzo ya kuelewana.
viongozi wa klabu za Simba SC na Young Africans SC kukaa chini na kumaliza suala la usajili wa mchezaji Hassan Ramadhani Kessy kwa njia ya mazungumzo ya kuelewana.
Hatua hiyo imefikiwa baada ya mjadala wa muda mrefu kuhusu kesi mbili
zilizofunguliwa na Simba mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na
Mwanasheria Richard Sinamtwa. Kesi ya kwanza iliyofunguliwa na Simba SC
ni dhidi ya Young Africans kudaiwa kuingia mkataba na mchezaji Hassan
Kessy wakati bado ana mkataba na Simba SC.
Kesi ya pili ni Simba SC dhidi ya mchezaji Hassan Ramadhani Kessy
kudaiwa kuanza kufanya mazoezi pia kusajili Young Africans na kwenda nje
ya nchi wakati akiwa ndani ya mkataba na Simba SC. Kama hawatafikia
mwafaka katika siku tatu walizopewa, mashauri hayo yatarudi mbele ya
kamati na kufanya uamuzi kwa mujibu wataratibu, kanuni na sheria
zinazoongoza mpira wa miguu Tanzania. Kupitia madai hayo, Simba inataka
kulipwa dola 600,000 za Marekani.
Wakati huo huo, kamati imeondoa kifungo cha mwaka mmoja kwa mchezaji
George Mpole wa Majimaji ya Songea baada ya klabu hiyo yenye maskani
yake Mkoa wa Ruvuma kufikia mwafaka Kimondo FC. Pia kamati iliridhia
mchezaji Enyina Darlington kutoka Nigeria kuanza kuitumika klabu yake
baada ya kukamilisha vibali vya ukazi na kufanya kazi nchini
vinavyotolewa na Idara ya Uhamiaji nchini katika Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi