Upungufu wa nguvu za kiume
unasababishwa na mambo mengi ikiwemo ukosefu wa virutubisho muhimu mwilini. Ni
jambo linaloweza kupata ufumbuzi kwa urahisi kama utazingatia kula vizuri na
kufanya mazoezi.
Ili kuongeza stamina kwenye mapenzi si lazima kutumia madawa
makali kama viagra au vilevi vikali.
Madawa na pombe hukupa nguvu zinazoisha
kwa muda mfupi, lakini hukuletea madhara makubwa yatakayokuandama kwa muda
mrefu zaidi. Ili kupata suluhishi la uhakika ni vizuri kuzingatia vyakula
vinavyoweza kukuongezea stamina na kujenga mwili wako vizuri na kukupa uwezo wa kufanya mapenzi vizuri zaidi bila kutumia "booster". Vyakula ni suluhishi maridhawa na asilia kwenye kila kitu maishani mwako.
Sababu za
kukosa nguvu za kiume
Ili kutatua tatizo ni muhimu kung’oa kabisa mzizi
wake. Mwili wako una maarifa ya kujirekebisha pasipo kuhitaji vilevi au
mawada, unachotakiwa kuzingatia ni chakula bora tu. Wahenga walisema, utakuwa bora kama chakula unachokula. Je wewe unakula chakula bora ili
kulinda heshima yako nyumbani?
Vitu vinavyoweza kupelekea kupungua kwa nguvu za kiume ni
kama:
·
Kutokuwa
na mzunguko mzuri wa damu mwilini, hasa sehemu za viungo vya uzazi kwa mwanaume.
·
Kutokuwa
na kiwango cha kutosha cha homoni ya Testosterone
·
Kupungukiwa
protini na hivyo kukosa amino asidi mwilini
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume
Leo napenda tuangalie vyakula ambavyo vinasaidia kuboresha
nguvu za kiume na kusaidia kwa kiasi kikubwa kudumisha mapenzi na kulinda
mahusiano na ndoa.
1. Blueberry
Blueberry
ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita
‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina
virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu
mwilini. Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume.
Vilevile,
blueberries zina nyuzinyuzi (fiber) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli
(Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na
mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu
zaidi.
2. Mtini (Figs)
Mtini
(figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo
kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za
kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au
kupungukiwa na nguvu za kiume.
3. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za
zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za
kiume.
Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na
nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na
nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa
nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya
mapenzi.
4. Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini.
Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri
mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
5. Vitunguu saumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko
mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye
uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
6. Ndizi
Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni
chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na
nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito. Ndizi ina kimeng’enyo cha
Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi (libido).
7. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi
kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato
kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid
huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.
Vyakula ni bora kuliko madawa makali
Mie binafsi nashauri kutumia njia asilia katika kutatua matatizo
yako yote ya kiafya. Mwili una njia zake za kurekebisha kila kitu. Ukiona kuna
tatizo inaashiria kuna upungufu ambao unatakiwa kurekebishwa. Kutumia madawa
makali hudhoofisha mwili na hivyo kuupunguzia uwezo wa kufanya kazi kama
inavyotakiwa. Ni vizuri kama utamuona daktari kama ukiona hakuna
kinachowezekana kabla hujaanza kutumia madawa.
Mara nyingi njia asilia hutumia muda mrefu sana kuleta mabadiliko,
lakini matokeo yake hudumu zaidi kuliko kutumia madawa makali ambayo hutibua
mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa mwili wako. Mie nashauri uangalie jinsi
unavyokula, nenda kapime vizuri. Kama jogoo ameshindwa kupanda mtungi, ruksa
kuangalia njia mbadala.
Ni vizuri kula kwa kiasi kabla ya kufanya mapenzi, hasa wakati wa
usiku kabla ya kwenda kulala. Kuvimbiwa husababisha mwili kufanya kazi ya ziada
ya kumeng’enya chakula hivyo kuingiwa na uchovu, uvivu na kunyong’onyea. Hii
husabisha kukosa usingizi na kupungua kwa umahiri wako katika kufanya shughuli
nyingi zinazohitaji nguvu, ikiwemo mapenzi, kwa ufasaha. Usije kumtafuta mchawi
wakati wewe ndio unajiroga, kuwa makini.
Kama ilivyo ada kwenye mambo mengi ya kiafya, hakuna muarobaini.
Ni vizuri ukajaribu kubadilisha chakula unachokula, fanya mazoezi mara kwa mara
ili kupata mwili wenye nguvu. Kama utakuwa na swali, weka maoni hapo chini nasi
tutakujibu bila kusika hukusu njia zaidi za kutatua tatizo la nguvu za kiume.