Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu.

Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.
1. Inaelezwa kuwa unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2. Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afyazaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya figo


Unywe kiasi gani? Jipatie kikombe kimoja cha juisi ya ubuyu kila siku hasa usiku na baada ya wiki kadhaa utaona matokeo yake mwilini.

Ili upate faida za juisi ya ubuyu, zinazoelezwa hapa, lazima upate ule ubuyu halisi (mweupe) usiochanganywa na kitu kingine cha kuongeza ladha au rangi. 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top