Unaweza kujiuliza kwamba Utafanya
nini iwapo umemuona yule aliyekupendeza katika mkahawa ama katika party
ulioalikwa na marafiki zako? Kama hujui la kufanya basi tumia macho yako kumtongoza
ili kumfanya avutiwe nawe kiurahisi.
Fanya kutumia mbinu hizi 10 kupitisha
ujumbe wako mara moja.
1. Mwangalie mara kwa mara
kikawaida
Umemuona yule aliyekupendeza? Fanya
kumuangalia mara kwa mara kikawaida. Itafikia mahali flani pia yeye atanotice
ya kuwa umekuwa ukimuangalia kwa muda hivyo utaiteka atenshen yake.
2. Badilisha kwa kuangalia
'kimukhtasari'
Usiwe na pupa ama utaonekana kama
stoka. Hivyo yule unayemzimia akikuona unamuangalia halafu aanze kukuangalia
kiudadisi, wewe mwangalie kwa sekunde moja halafu ghafla angalia kando.
3. Rudia kumuangalia
Mtizame tena unayemzimia. Mwangalie,
lakini angalia kando mara moja wakati ambapo atakuangalia. Usizubae, mwangalie
tena kwa sekunde nyingine moja kwa mara nyingine.
4. Mfanye ajue kuwa yuko
akilini mwako
Mara ya kwanza, unayemzimia ataona
ya kuwa kumuangalia yeye ilikuwa tu ni kupita njia. Lakini wakikushika mara kwa
mara unawaangalia wataanza kuingiwa na hisia ya kuwa wewe umevutiwa nao.
Usimwangalie zaidi ya sekunde moja ama utaua msisimko ambao unaanza kujenga
kati yenu.
5. Jenga msisimko
Ok kufikia sasa itakuwa umeteka
atenshen ya yule umemzimia na mara kwa mara atakuwa akikuangalia kuchunguza
iwapo unamuangalia au la, sasa kilichobaki nikujenga msisimko. Jizuie kumwangalia
kwa madakika.
Kufanya hivi kutamfanya yule
unayemwangalia kutaka kujua kwa nini umeacha kumuangalia hivyo atakuwa mara kwa
mara akikuangalia ili kuhakikisha ya kuwa unamuangalia au la. Mbinu hii
inamfanya pia yeye kuingiwa na msisimko wa kuendelea katika huu mchezo.
6. Fanya mjeuko
Umemnotice yule unayemzimia yuko
pembeni mwa jicho lako. Mwangalie bila kujeuza kichwa chako. Ngojea mpaka ule
wakati atakapokuangalia. Ukimwona anakuangalia, fasta jeuka uanze kumuangalia.
Kufanya hivi kutakuwa kunaleta dhana ya kuwa ni yeye ndiye anayekuangalia na
wala si wewe. Pia inaleta dhana ya kuwa wao ndio wamevutiwa na wewe na wala si
kivingine.
7. Mwangalie kwa muda
mrefu
Kufikia sasa mumekuwa mkibadilishana
macho kimukhtasari na yule unayemzimia. Sahizi atakuwa anakungojea umuangalie
kwa mara nyingine. Well, wakati huu wakati ambapo utamwangalia, mwangalie zaidi
ya sekunde moja halafu angalia kando.
8. Tabasamu na tahayari
Ongea na marafiki zako ama jikeep
buzy, halafu mwangile sekunde moja au mbili. Na kila mara utakapomwangalia
tabasamu ama tahayari kikawaida. Usitabasamu kama unamwangalia. Ngojea mwanzo
mpaka uangalie kando halafu ndipo utabasamu.
9. Angalia mwitikio wake
Ok je huyu unayemuangalia pia yeye
anakuangalia mara kwa mara? Kama jibu ni ndio, basi mbinu hii inafanya kazi na
inaonyesha dalili ya kuwa siku yako itakuwa ya furaha na haitapotea hivi hivi.
Iwapo itatokea huyu unamwangilia haonyeshi dalili zozote za majibu, ni dhahiri
ya kuwa hujawavutia hivyo ni vyema ujiondoe ama ujipatie shughli mbadala.
Hauwezi kushinda wakati wote katika mchezo wa kutongoza kwa macho.
10. Tabasamu
unapomwangalia
Kufikia sasa unauhakika ya kuwa huyu
unayemwangalia mara kwa mara anaonyesha dalili ya kupendezwa nawe. Hatua
utakayoichukua sahizi hakuna cha kurudi nyuma. Katika moja wapo ya kumwangalia,
mwangalie direct kwa macho yake halafu vuta tabasamu refu. Kama pia atajibu kwa
kutabasamu, utakuwa umeufunga mchezo. Iwapo unayemwangalia atakuangalia na
mshangao basi anahitaji muda kiasi kabla kufanya approach ya mwisho.
Kama huu mchezo umefaulu kwako, hivi
ndivyo unavyopaswa kufanya. Kama wewe ni mwanamke mpatie nafasi ya huyo
mwanaume aongee na wewe. Na kama wewe ni huyo mwanaume wangojea nini? Chukua
hatua ya haraka
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv