Hivi viungo huwa tunavitumia kila siku au mara kwa mara (kwa wale wanaojua kucheza na kuitumia vilivyo miili ya wapenzi wao) wakati tunafanya mapenzi na cha kushangaza huwa tunavitumia kufuata “mtiririko” wake yaani kama vilivyo pangwa iwe kuanzia juu kwenda chini au chini kwenda juu.
“Vifaa” hivi humpa mpenzi raha Fulani ya kimapenzi na vilevile humuongezea hamu ikiwa vitatumiwa vizuri . Ikiwa unafahamu umuhimu wake katika kufanya mapenzi nakupongeza na nitahitaji nyongeza ya maelezo yako na ikiwa hujui basi endelea kuwa nami ili tujifunze sote….Leo nitazungumzia juu ya nywele tu.
NYWELE:
Nywele ni sehemu muhimu sana ya urembo wa mwanamke kama ilivyo sehemu nyingine za mwili wake na wakati huohuo nywele hizo zinachukua nafasi kubwa ktk mapenzi na huongeza raha na mvuto kwa mpenzi wako hasa kama mnatoana jasho wakati mnafanya mapenzi.
Nywele za mwanamke hupendeza zaidi machoni kwa mwanaume/mpenzi wako mara baada ya kufanya mapenzi kuliko zinavyokuwa mara baada ya kutoka kwa “hairdresser/Salon”.
Mwanaume hufurahia kucheza na kichwa cha mwanamke nakuhisi ule mkwaruzo wa nywele, harufu yake asilia iliyochanganyikana na mafuta, sabuni au “shampoo” (hivyo hakikisha hupaki mafuta yenye harufu kali kichwani).
Inasemekana wanaume wengi hupenda kushika kichwa cha mwanamke wakati wa kufanya mapenzi au kuchezeana na hukosa raha fulani ikiwa watawekewe mipaka kuwa wasiguse kichwa kwa vile wataharibu mtindo wa nywele uliogharamia “Salon”.
Sina shaka umeshawahi kusikia baadhi ya wanaume wakilalamika kuwa hawapendi wake/wapenzi wao wavae “wigs” kitandani kwa vile wanashindwa kucheza na vichwa vyao, sina hakika na wale wanawake wanaoondoa nywele zote kichwani.
Mwanamke na nywele za mpenzi wake:
wanawake wote wanavutiwa na nywele za vichwani mwa wanaume bali huvutiwa na nywele sehemu nyingine za mwili kama vile kwapani, usoni (nyusi, ndevu n.k ), kifuani, sirini na kwingineko .
walio wengi wanavutiwa sana na nywele za usoni (zinafanya wanahisi wako na Real man) na zile za miguuni hasa wakati wanatoa “massage” ya miguu kwa mpenzi, ule mkwaruzo wake huwapa raha ya ajabu na kuwafanya wafurahie kufanya wanachokifanya kwa wakati huo ambacho ni kumkanda miguu yake, vilevile wanapenda kucheza na zile za sirini wakati wa maongezi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv