UJAUZITO ni safari ndefu inayomchukua mwanamke
miezi tisa au majuma arobaini hadi kujifungua. Ni safari yenye mikikimikiki na
hatari nyingi kwa mama na mtoto. Tusichukulie suala la ujauzito kama jambo la
kawaida ingawa pia ni wajibu kwa mwanamke. Ujauzito siyo hali ya hatari au kutisha
endapo mambo ya msingi yatazingatiwa kabla ya kuwa mjamzito na kipindi cha
ujauzito hadi baada kujifungua.
Katika kipindi cha ujauzito kuna mambo
mengi ambayo ni mabadiliko humtokea mama na mtoto aliye tumboni.
NINI CHA KUFANYA KATIKA KIPINDI HIKI?
Ni vyema upange sasa unataka kuwa mjamzito
au mwezi fulani unataka kushika mimba, uwe na mpango. Hata hivyo, hakikisha
umri wako upo zaidi ya miaka 20 kwa usalama zaidi wa afya yako. Mshirikishe
mwenzi wako na mwambie ungependa upate ujauzito, siyo vizuri kushtukiza kwani
inaweza kukupa ‘stress’ wewe mwenyewe au mwenzako endapo mmoja wenu hajajiandaa
kisaikolojia.
CHEKI AFYA YAKO
Hakikisha una afya njema, huna magonjwa
sugu kama kisukari, shinikizo la damu, magonjwa mengine ya moyo, kansa, HIV,
kifafa, pumu, siko seli au grupu lako la damu ni RH Negative.
Endapo una matatizo haya hapo juu, basi
haraka wasiliana na daktari wako wa masuala ya uzazi akupe ushauri kwani
magonjwa mengine yatakusumbua wakati wa ujauzito, au magonjwa yenyewe
yatamwathiri mtoto.
Hakikisha huna magonjwa au matatizo katika
viungo vya uzazi, mfano kutokwa na uchafu ukeni wenye muwasho na harufu mbaya,
vipele au vidonda sehemu za siri, maumivu wakati wa tendo la ndoa, kutokwa na
damu au usaha ukeni. Vile vile mfumo wako wa uzazi uwe vizuri, matatizo katika
mfumo wa uzazi ni kama vile maumivu ya tumbo chini ya kitovu, kuvurugika kwa
mzunguko wa hedhi, kutopevusha mayai na kukosa hamu ya tendo la ndoa.
ACHA VILEVI
Epuka unywaji wa pombe na uvutaji wa
sigara, hili hata kwa mwanaume anayetaka mtoto. Mwanamke kabla ya kuwa mjamzito
hakikisha unakula sana mboga za majani ili upate kiwango kizuri cha vitamin ya Folic
Acid, ni vema ule sana
mboga za majani au upate virutubisho vya Folic Acid. Endapo hutakuwa na kiwango kizuri cha Folic
Acid, kuna hatari ya
kuzaa watoto wenye matatizo.
MAZOEZI
Fanya mazoezi mepesi mara kwa mara ili
kuimarisha nyonga na viungo vyako vingine na usipate matatizo wakati wa
kujifungua. Pata ushauri wa daktari kipindi muafaka.
Tibu magonjwa yanayoathiri mfumo wa uzazi,
mfano maumivu ya korodani, maumivu ya njia ya mkojo, upungufu au ukosefu wa
nguvu za kiume. Kutoa manii mepesi sana kiasi kwamba baada ya tendo la ndoa
manii zote zinatoka ukeni.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv