Nikukaribishe sana msomaji wa edonetz katika
makala za leo na leo tumuangazie muigizaji wa filamu ya jesus na Yesu Kristo
aliyekuja duniani takribani miaka 2000 iliyopita.edonetz leo inakuletea
historia ya mtu ambaye ameigiza filamu ya Yesu inayofahamika kwa jina la
''JESUS'' ambayo iliigizwa mnamo mwaka 1979 huko nchini Israel, GK imeamua
kufanya hivi baada ya kuona ni kwa jinsi gani filamu hiyo imekuwa ikigusa
maisha ya watu wengi kiasi kwamba baadhi ya watu wanasahau kwamba mtu aliyemo
kwenye filamu hiyo ni mwigizaji tu na siyo Yesu.hata yeye amekiri kwamba wakati
wa uigizaji alikuwa akisuluhisha mambo yaliyokuwa yakijitokeza yeye na
waigizaji wenzake baada ya wao kusahau kwamba yeye si Yesu bali anaigiza tu.
KARIBU.
Brian Deacon ndio jina lake mwigizaji huyo
ambaye ni mwingereza aliyezaliwa mnamo tarehe 13/02/1949 huko Oxford nchini
Uingereza akiwa ni mtoto wa pili katika familia yao baba yake akiwa fundi
makenika na mama yake akiwa ni nesi ndoa yake ya kwanza na Rula Lenska
ilivunjika ambapo alizaa na mkewe huyo binti yao aitwaye Lara Deacon,ndoa yake
ya pili alioana na mwanamama Natalie Bloch mnamo mwaka 1998 mpaka sasa wapo
kwenye ndoa hiyo.
Aliigiza filamu ya Yesu ambayo pia ilimfanya
aokoke mara baada ya kuitazama akiwa na miaka 30,baada ya kupita kwenye mchujo
mkali wa waigizaji zaidi ya elfu moja ambao walifanyiwa mahojiano huku 260
wakijaribishwa kuigiza (screen test) kuona
kwamba wanafaa akiwa ni mwingereza pekee kati ya waigizaji Waisrael walioingia
kwenye usaili huo akiwa chini ya kampuni iitwayo New shakespears ambako alikuwa
akifanya sanaa za majukwaani na uigizaji.
Brian Deacon miaka
iliyofuatia baada ya kuigiza kama Yesu.
Anasema kabla ya kuchaguliwa mtihani wake wa
kwanza ulikuwa kutoka kwa wakala wake aliyemvunja moyo kwakumweleza hadhani
kama yeye (Brian) atafaa kwenye kumwigiza Yesu,lakini anasema alifanikiwa,baada
ya hapo akawa na wakati mgumu kutoka kwa watu ambao kila mmoja alikuwa
anajaribu kumweleza jinsi anavyotakiwa kuigiza,sauti yake na mambo
mengine,ingawa yeye alisema nitatumia sauti yangu na maelezo kutoka kwa
muongozaji.Amesema wiki tatu kabla hawajaanza kurekodi filamu hiyo alisoma
kitabu cha Luka mtakatifu zaidi ya mara 20 kwakuwa filamu hiyo imenukuliwa
kutoka kitabu hicho ambapo Brian amesema kusoma kwake kulimpa nguvu sana na
moyo wa kuigiza filamu hiyo na kuweza kumfahamu vyema Yesu kuwa ni mtu wa aina
gani.
Katika miezi saba waliyochukua kuigiza filamu
hiyo Brian amesema,walikuwa wanaigiza kwa masaa mengi kuanzia saa kumi za
alfajiri mpaka mwisho wa siku kiasi kwamba wakati mwingine aliwaambia wenzake
kwamba wamsaidie kwani amechoka sana hajui kwamba angeweza kuigiza kwa
siku hiyo lakini anasema alikuwa anashangazwa na nguvu za ajabu alizokuwa
akizipata na kuendelea kuigiza ingawa wakati huo anasema alikuwa mkristo jina
wa kanisa katoliki,alikuwa anauwalakini kuhusu mafundisho na huduma ya Yesu kwa
ujumla,siku moja wakati anaigiza alikuwa anawaombea watu mara mwanamke mmoja
alishika mkono wake kumbe alikuwa na mapepo alimuombea na mapepo yalimtoka
mwanamama huyo.
Siku nyingine waliokuwa wakiigiza kama
wanafunzi wa Yesu wapatao 12 wakiwa ndani ya basi walikuwa wamepanga kugoma
kutokana na malipo waliyokuwa wakipata cha ajabu Brian anasema director alikuja
kumuomba yeye (Brian) azungumze nao warejee kazini akashangaa akamwambia mimi
sio Yesu ni Brian Deacon, akaamua kuzungumza nao, baada ya masaa 36 walikubali
kurudi kuendelea na kazi.
Amesema mtihani mwingine ni siku alipokuwa
hotelini Tel Aviv ghorofa ya 18 usiku mara kukawa na moto hotelini hapo baada
ya mwingereza mmoja aliyekuwa akivuta sigara kusahau kuizima hivyo kusababisha
moto,lakini anasema bahati nzuri hakuna aliyejeruhiwa ila walifanya kazi siku
inayofuatia muda mrefu bila muongozaji kujali kwamba hawakulala vyema usiku.
Amesema siku hiyo mmoja wa waigizaji
anayeitwa Tom Panella alianzisha mada kwa kusema moto uliokuwa umetokea ni hila
za shetani,na kusababisha mjadala wa muda mrefu ni vipi shetani anahusishwa
kwenye swala hilo lakini jibu likawa,shetani hataki filamu hiyo irekodiwe ndio
maana analeta hila zake.haikuwa kazi rahisi kurekodi filamu hiyo na pia si
ujuzi wa kufurahia,baada ya kumaliza kurekodi kwa takribani miezi 18 ilianza
kuonyeshwa kwa baadhi ya watu na ndipo hata yeye kwa mara ya kwanza akaona ni
kwa jinsi filamu hiyo ilivyonanguvu,ukweli na kugusa mioyo ya watu.
Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi
kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu
kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika
nchi 133 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua
kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini
ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini
Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa
katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa.
Brian anawaambia watu kwamba yeye ni
mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo
ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru
kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema
anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo
kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na
kubadilisha maisha ya watu.
Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja
na A zed & Two Noughts ya mwaka
1985, The Feathered Serpent ya
mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie
iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank
Miles.
Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa
filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. Habari kwa msaada wa mtandao.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv