Ni wazi kwamba kuna wanaume wengi ambao huanza na gia kubwa ya maneno hao wamebainika kupoteza mvuto wa kimapenzi waliokuwa nao mwanzo kwa wapenzi wao.
Hakuna shaka kwamba, katika mazungumzo ya awali ya mwanaume anayemteka mwanamke kimahaba, kinywa chake huwa hakikauki maneno haya manne zenye nguvu ya kumdatisha mwanamke, ambazo ni NAKUPENDA, NAKUHITAJI, SAMAHANI na ASANTE. 
Walio wengi ujaribu kutafuta maneno mengi tu ili kukubaliwa lakini ukitumia vizuri maneno haya yana umuhimu mkubwa sana katikamahusiano hebu tukayajadili..
TUANZE NA NENO NAKUPENDA. neno la kwanza lenye nguvu ya kumteka kimapenzi mwanamke ni nakupenda. Neno hili ni tiba inayoponya hofu na kumfanya mwanamke ajiamini. Hila neno hili kwa sasa watua wameanza kulitumia kikawaida nakupelekea hata wanaoambiwa hulichukulia kawaida yaani limeshushwa thamani ila ni neno lenye maana sana
NAKUHITAJI. wakati wa kutongoza, mwanamke anapenda kuambiwa neno hilo na kufanyiwa vitendo inavyoonesha kuhitajika kwake katika maamuzi, matembezi, faraja na muongozo wa kimaisha.

ASANTE ni neno dogo kutamkika lakini linasumbua wengi na lina maana kubwa , Sambamba na hilo mwanamke anapenda sana kupewa asante katika yale anayofanya penda sana kutumia neno hilo.

SAMAHANI. Ndugu zangu kuna wanaume ambao hawako tayari kuomba msamaha kabisa hata kama wamekosa kosa kubwa na la wazi kiasi gani? Kifupi tabia hiyo haipendezi. Ni busara kwa mwanaume kumuomba radhi mpenzi wake, ili naye ajione ni mwenye mamlaka na hivyo kuzidisha upendo na uangalizi wa tabia mbaya za mwanaume.
 

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top