Kwenye chai na kahawa
kuna kitu kinaitwa CAFFEINA/KAFEINA.
1. Kafeina ni madawa ya kulevya kundi la ‘Stimulants
drugs’.
Hii ndiyo sababu kwa mtu
aliyezoea kunywa chai hii kila siku au kahawa, siku asipokunywa kichwa humuuma,
ni kwa sababu amekuwa mtegemezi au teja wa kafeina.
Kafeina ni kiungo mhimu
karibu katika soda zote zenye rangi nyeusi. Kafeina huongezwa pia katika baadhi
ya dawa za kupunguza maumivu mwilini.
Kwahiyo Kafeina ambayo
hupatikana katika chai na kahawa ni aina mojawapo ya madawa ya kulevya.
2. Kafeina ni kikojoshi (diuretics).
Ukinywa kikombe kimoja
cha kinywaji chenye kafeina yaani chai au kahawa, basi muda si mrefu utaenda
kukojoa vikombe viwili. Kwa
sababu kafeina ni taka isiyotakiwa mwilini, mwili utafanya kila
uwezalo ikibidi ujikamuwe wenyewe kupata maji ya
ziada kuweza kuitoa kafeina hii uliyoinywa kwa kisingizio cha chai, kahawa au
soda.
Madhara yake ni Moja; kama
unakunywa kinywaji na muda si mrefu unalazimika kwenda kukitoa inamaanisha
kinywaji hicho hakikutumika vema na mwili. Pili; kumbuka ulikunywa kikombe kimoja na umeenda kutoa viwili,
hivyo umekopwa maji mwilini mwako na ukumbuke kuwa MAJI NI UHAI.
Seli ndani ya mwili
lazima zibaki katika kiasi kidogo cha alkalini kutoka
7.2 mpaka 7.4, wakati 7.0 ni ya
kati au husemwa sifuri katika kipimo cha PH (potential hydrogen). Chini ya 7.0
ni asidi na juu
ya 7.0 ni alkalini. Kafeina yenyewe ni asidi, hivyo ikiwa mtu
anafanya chai au kahawa ndivyo vinywaji vyake vya kila siku basi mtu huyo
lazima atakuja kupatwa na kansa katika siku za usoni kwakuwa seli za kansa
huishi katika hali ya uasidi pekee na kafeina ndimo mazingira mazuri ya kuishi
asidi.
Jarida moja la afya la
Uingereza, ‘The British Medical
Journal Lancet’, limeripoti uhusiano mkubwa uliopo baina ya utumiaji wa
kahawa na kansa ya kibofu cha mkojo na kupungua kwa uzarishwaji wa mkojo.
4. Kaffeina huchangia upotevu wa madini na vitamin mhimu
mwilini.
Kafeina ambayo ni
kikojoshi, huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka na kuziacha seli
bila muda wa kutosha kuyatumia maji hayo, maji yanapokimbia kwa haraka nje ya
mwili huyakimbiza pia madini mhimu nje ya miili yetu.
Mwili una vyanzo 3 vya
nguvu ambavyo ni Sukari, Mafuta, na Maji/Chumvi. Tumesema kaffeina ni
kikojoshi, hivyo kaffeina hupelekea upotevu usio wa lazima wa maji mwilini,
mwili unapokosa maji kama chanzo chake cha nguvu, moja kwa moja huhamia
kuitegemea sukari kama chanzo chake cha nguvu na mwishowe kisukari lazima kitokee.
6. Uchovu sugu.
Wapenzi wengi wa chai ya
rangi na kahawa mara nyingi wanapojisikia uchovu hukimbilia kikombe cha kahawa
au chai. Kaffeina iliyomo katika chai au kahawa huenda kuiamsha na kuitumia
nguvu iliyokuwa imehifadhiwa na mwili kwa ajili ya matendo ya dharura na
kukuacha wewe ukiwa huna nguvu ya ziada kwa ajili ya kazi za dharura, matokeo
yake ni mwili unakuwa upo katika hali ya msukosuko muda wote.
Utolewaji wa sukari
iliyokuwa imehifadhiwa, kunapelekea mfadhaiko mkubwa kwenye mfumo wa
dharura wa mwili. Unaposhitushwa kidogo tu, unakuwa na nguvu za haraka (Unahamaki) kushughurika na tatizo.
Hali hii hatimaye inaweza kupelekea kukauka kwa tezi ya adreno
kutakakosababisha damu chache yenye sukari (hypoglycemia), udhaifu, na kuumwa sana iwapo sukari
haitachukuliwa mapema kupandisha juu damu sukari.
Kwa sababu ya biashara
kuunda vyakula vyetu vyote maalumu na vinywaji vyenye radha mpya, radha nzuri
na nguvu ya kutosha kwa kutumia kafeina toka katika mimea na
mitishamba kama vile ginseng kuisisimua tezi ya adreno,
kunasababisha Ini kutoa sukari iliyokuwa imehifadhiwa mwilini kwa ajili ya
matumizi yake ya dharura.
7.Imethibitika pia kuwa kafeina imekuwa ikiingilia na kuathiri
unakilishaji wa
kinasaba (DNA),
Namna ambavyo seli mpya hutengenezwa. Kafeina
inaweza kusababisha upotevu toka mwilini wa vitamini nyingi za kundi B, kundi
C, zinki, potasiamu na madini mengine. Kahawa huongeza hali ya uasidi kwenye
utumbo mdogo.
8. Kafeina inaweza kusababisha msukosuko ndani ya mwili.
Kafeina siyo kwamba tu
huimaliza nguvu iliyokuwa imehifadhiwa kwenye ubongo, bali pia huzuia mfumo
vimeng’enya katika kutengeneza kumbukumbu kwenye ubongo.
Kituo cha Sayansi kwa
maslahi ya umma (Center
for Science in Public Interest) kimewashauri kinamama
wajawazito kukaa mbali na kafeina kwa kuwa tafiti zimeonesha kwamba kiasi cha
kafeina kilichomo kwenye vikombe 4 vya kahawa kwa siku kinaweza kusababisha
matatizo wakati wa kujifungua kama yalivyoonwa katika majaribio kwa wanyama.‘Madawa na wewe’,
Kwa mjibu wa Dr. Earl Mindell,
mwandishi wa kitabu; ‘Earl
Mindell’s New Vitamin Bible’ (zaidi ya nakala milioni 10 zimeuzwa), anasema katika ukurasa wa
414 wa kitabu hicho kuwa ‘kafeina ni dawa yenye nguvu kubwa, uwezekano ni kuwa,
hauifurahii tu kahawa au cola yako ya kila siku, bali umekuwa mtegemezi
au teja (addicted) wa hiyo kafeina’.
Madhara ya chai ya rangi
na kahawa mwilini ni mengi sana na tatizo moja litapelekea lingine na orodha
inakuwa haiishi.
NAMNA YA KUEPUKA KAFFEINA KWENYE KAHAWA NA CHAI:
Badala ya kutumia majani
hayo ya chai meusi, wewe chemsha maji yako ya chai kama kawaida na unaweza kutumia vifuatavyo kukamilisha chai yako;
unaweza kutumia tangawizi
na kumbuka pia tangawizi ni dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini.
Kwahiyo unapoinywa chai
ya tangawizi siyo tu unaepuka madhara ya kaffeina peke yake, bali pia unakuwa
umekunywa dawa ya zaidi ya magonjwa 72 mwilini!. Unaweza pia kuweka mdalasini,
mchaichai, kukamulia ndimu,
pia unaweza kutumia mchanganyiko wa viungo vingi vya chai (spiced tea) ambavyo vinapatikana kwa
wingi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv