Kuna athari kubwa sana zinazotokana na utafunaji wa bigijii (chewing gums) kwa muda mrefu. Utafunaji huo husababisha tumbo kuzalisha acid ya kutosha likifikiri kuna chakula ambacho kinatafunwa tayari kumezwa. Kitendo cha kutafuna bigijii husisimua seli linazozunguka ukuta wa ndani wa tumbo kutengeneza juisi (digestive juice) ambayo husaidia kwenye mmeng’enyo wa chakula.
Hii ni njia asilia ambayo husababisha chakula ambacho kimetafunwa kuanza kumeng’enywa punde tu kinapofika tumboni. Kwahiyo utafunaji wa bigijii (chewing gums) husababisha uzalishaji wa aside isiyo na ulazima. Hii ni habari nmbaya kwa walaji wa bigijii kwani aside hii huongeza athari za kupata vidonda vya tumbo.

Lakini risk ni ndogo sana labda uwe unatafuna bigijii (chewing gums) nyingi sana kwa siku, kwahiyo ondoa hofu labda uwe kocha wa mpira wa miguu (football coach).
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top