Mwanamitindo Hanne Gaby Odiele amefichua kwamba
alizaliwa na jinsia mbili. Gaby mwenye umri wa miaka 28
anasema kuwa ameamua kutangaza jinsia yake ili kuhamasisha watu kuhusu watu
wenye jinsia mbili mbali na kutoa hamasa kwa jamii.
Ni miongoni mwa wanamitindo wa hadhi ya juu
kuzungumzia kuhusu jinsia yake.
Watu
wenye jinsia mbili hawana viungo vya ndani ama vya nje vinavyowatambulisha moja
kwa moja kuwa na jinsia ya kiume ama ile ya kike.
''Nimefikia wakati katika maisha yangu ambapo
nimeamua kutangaza jinsia yangu'', alisema
Hanne.
''Ni wakati wa watu wenye jinsia mbili kujitokeza,
kuondoa uoga na kuzungumzia maswala ambayo yalitukumbuka tukiwa watoto''.
Hanne
ameshiriki katika kuuza mitindo ya Chanel na Prada na pia amekuwa katika kampeni
za Mulberry na Balenciaga.
Katiika
kanda za video zilizochapishwa katika mtandao wake wa Instagram ,anaelezea
kwamba licha ya kuzaliwa na jinsia mbili hajashindwa kupigania kazi yake katika
sekta ya mitindo.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv