unaweza kuifanya ngozi yako ianze kuonekana kuwa ya ujana, yenye mng’aro na laini kwa kutumia mbinu za asili.

Mahitaji

-Kipande cha papai
-Maji safi ya kunywa glasi 8
-Nyanya mbili
Namna ya kufanya

Chukua papai lililoiva, limenye kisha liweke kwenye blenda kwa ajili ya kulisaga kupata ujiuji mzito. Baada ya kutengeneza ujiuji huo, jipake usoni na acha ukauke kwa muda wa dakika kumi na tano. Osha na maji ya uvuguvugu kisha kausha uso wako.
Unaweza kurudia zoezi hili mara mbili kwa siku, kwa muda wa wiki mbili hadi tatu, utaona matokeo yake. Angalizo: Unapofanya zoezi hili, lazima pia uwe na utaratibu wa kunywa maji safi mengi, kwa angalau glasi nane kila siku.

Mwili unapokuwa na maji ya kutosha, hata ngozi huwa na afya njema. Kila mtu anashauriwa kuwa na kawaida ya kunywa kiasi hicho cha maji, kwa siku zote za maisha yake.

Mbadala wa kutumia papai, unaweza kutumia nyanya mbivu. Cha kufanya, ni kama vile ulivyofanya kwenye papai, menya nyanya kisha ziweke kwenye blenda, saga kupata juisi nzito. Tumia juisi hiyo kujipaka usoni, asubuhi na jioni kulingana na ratiba yako. Ukishapaka, acha ikauke kwa dakika kumi na tano kisha osha kwa maji ya uvuguvugu na rudia zoezi kwa wiki mbili hadi tatu, utaona matokeo.
Unapotumia mbinu hizi za asili, epuka kuendelea kutumia krimu au mafuta yenye kemikali, tumia mafuta ya kawaida tu na utaona ngozi yako inavyopendeza.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog na  youtube@edone tv
 
Top