Zingatia vyakula hivi ni mhimu sana kwa wenye afya
mbovu, kuwa na nzuri ni hivi vifuatavyo.
SAMAKI: Wana
virutubisho aina ya Omega 3 ambavyo huulinda moyo dhidi ya maradhi, humuongezea
mlaji uwezo wa kukumbuka memory, kuna virutubisho vyenye uwezo wa kupambana na
kansa mwilini, kuongeza kinga mwilini na kuondoa mafuta mabaya mwilini bad
cholesterol.Pia wana virutubisho muhimu kama vile vitamini D, vitamin 12,
vitamini B3, vitamini B6, Omega 3 Fatty acids, protini na madini mengine mengi.
TANGO: Husaidia
kusaga chakula tumboni hivyo kumuwezesha mlaji kupata choo laini pia linaweza
kutumika katika kuboresha ngozi ya uso kwa kupaka na huondoa vipele na kuifanya
ngozi kuwa nyororo. Ni zuri linapoliwa na maganda yake na unaweza kula kiasi
utakachoweza. Pia kula asali na tende.
MAHARAGE
YA SOYA: Faida yake ni kushusha shinikizo la damu, kuimarisha sukari
mwilini, kupambana na ugonjwa wa kisukari, figo, moyo, kutoa kinga dhidi ya
ugonjwa wa kansa ya kibofu na magonjwa mengine ya wanawake.
KAROTI: Miongoni
mwa faida nyingi za karoti mbichi au zilizochemshwa ni pamoja na kushusha
kolestro mbaya mwilini, kupunguza unene, kuimarisha nuru ya macho, kuimarisha
shinikizo la damu, inatoa kinga kwenye figo na inaimarisha sukari mwilini.
PAPAI,
TIKITIMAJI: Ni matunda muhimu mwilini ambayo hata mgonjwa wa kisukari
anashauriwa kuyala kwani yana kiwango kikubwa cha ufumwele fibre, huimarisha
kiwango cha sukari mwilini. Kula moja katika ya matunda hayo mawili, kila siku.
KITUNGUU
SAUMU: Husaidia kuyeyusha damu mwilini hivyo kumuepusha mlaji
kushikwa na ugonjwa wa moyo pamoja na presha, pia hutoa kinga kwenye ini na
huondoa maumivu ya viungo. Kula angalau kitunguu kimoja mara moja kwa wiki.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv