Miguu kutoa harufu mbaya ni moja ya matatizo ambayo huwasumbua watu wengi hususani wanaume wengi katika jamii.
Tatizo hili mara nyingi huwakwaza zaidi wale ambao huishi karibu na watu wenye shida hiyo kutokana na kuwa watu wengi wenye tatizo hili huwa wagumu kukubaliana na hali yao.
Zipo sababu kadhaa ambazo huelezwa kuchangia tatizo hilo, lakini sababu kubwa zaidi ni uchafu  na  ndiyo chanzo kikuu cha miguu kutoa harufu.
Kwa kiasi kikubwa uchafu huo ndio unasababisha kuzaliwa kwa vijidudu vinavyoleta harufu mbaya kwenye miguu.
Licha ya kuwepo kwa tiba mbalimbali ambazo mtu mwenye tatizo hili anaweza kutumia, lakini tiba kubwa zaidi ni ile ya usafi ni jambo kubwa analopaswa kuzingatia mtu mwenye tatizo hili.
Unashauriwa kuwa uwapo na tatizo hili unapaswa kuzingatia kusafisha miguu yako mara kwa mara na ukiiacha mikavu muda wote ili kuepusha unyevunyevu.

Pia unapovaa viatu vya kufunika hakikisha unavaa soksi safi na kavu na uepuka kurudia soksi au kuvaa ambazo hazijakauka vizuri kwani zinaweza kusababisha miguu kunuka mara dufu.
Usivae viatu vilivyoloa na endapo ikatokea umenyeshewa, hakikisha unavianika kwenye hewa ili vikauke na kupunguza uwezekano wa kutokea harufu.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog na  youtube@edone tv
 
Top