Kama wewe unajiuliza kuwa kuna faida na madhara
gani kwa wapenzi kuachana kisha kuja kurudiana tena na kuanzisha upya uhusiano
wa kimapenzi? Ukiwaona watu wanaoishi kwenye aina hii ya uhusiano wa kimapenzi
unawachukuliaje? Twende pamoja.
Aina hii
ya uhusiano wa kuachana na kila mmoja akaendelea na maisha yake kisha baada ya
muda mkarudiana tena, likaonekana jambo la ajabu au geni katika mila na desturi
za Kiafrika lakini, hili ni jambo la kawaida kabisa katika uhusiano wa
kimapenzi duniani kote.
Takwimu zinaonesha kwamba asilimia kubwa ya
wanandoa au watu ambao wapo kwenye uhusiano imara wa kimapenzi, wamewahi
kupitia kipindi hiki kigumu cha kutengana na kurudiana, wengine wakifanya hivyo
mara kadhaa.
Baadhi ya
watu ambao baada ya kutengana, hushindwa kukaa chini na kumaliza tofauti zao
hata kama bado wanapendana kwa kuona jamii itawashangaa kuwaona wakiwa pamoja
tena baada ya kuachana kwa kashfa na vurugu kubwa.
TUANZE
NA MADHARA YAKE
Madhara yanayowakumba watu wanaoishi kwenye aina
hii ya uhusiano. Inapotokea mmeachana na kila mmoja akaanzisha ukurasa mwingine
wa mapenzi, lazima atakutana na mazingira tofauti kabisa na yale mliyozoea
kuishi pamoja. atakutana na mtu mwingine ambaye amekuzidi vitu vingi, hata
ikitokea wakaachana na akarudi kwako, hawezi kukupenda kwa kiwango kile kama
ilivyokuwa mwanzo kwa sababu tayari kuna vitu vipya vimeingia ndani ya kichwa
chake na huo utakuwa ufa mwingine ambao hapo baadaye utasababisha muachane
tena.
Kitu
kingine ni maradhi. Ni hatari kurudiana na
mwenzi wako kwa sababu hujui baada ya kutengana na wewe alikuwa akitoka na
nani. Ni rahisi kukuletea maradhi ya zinaa au Ukimwi hasa kama alikuwa anatoka
na watu wasio sahihi.
Kitu
kingine ni Kulipizana visasi nalo ni tatizo lingine linaloweza kuwakumba watu wanaoishi kwenye
uhusiano wa aina hii. Yawezekana wewe ndiye uliyemuumiza mwenzi wako wakati
mnaachana, ukautesa moyo wake na kushindwa kumuonea huruma wakati akiteseka. mnaporudiana,
wengi hubaki na vinyongo ndani ya mioyo yao na kwa sababu wewe ndiye
uliyemuumiza na yeye atakutafutia sababu ya kulipa kisasi ili na wewe uhisi
maumivu kama aliyoyahisi yeye wakati mnaachana.
TUANGALIE
FAIDA ZAKE
Tayari mnajuana:
Unapoanzisha uhusiano mpya, unaweza kudhani kwamba
unampenda sana mtu uliyenaye kwa sababu bado humfahamu kwa kina lakini
ukishamjua kwa undani, hasa tabia zake, yale mapenzi uliyokuwa nayo huisha
haraka kwa sababu ya upungufu utakaoubaini. Ila Unaporudiana na mwenzi wako,
huanzi upya kwa sababu kama ni kumjua tayari unamjua na yeye anakujua, unaelewa
udhaifu na uimara wake, hali kadhalika na yeye anakujua kwa hiyo mkiamua kuwa
‘serious’, kazi inakuwa nyepesi kuliko kuanza upya na mtu mwingine.
Mmeshakomaa kihisia:
Kumrudia mtu aliyewahi
kukuumiza, huhitaji ujasiri mkubwa sana na ukiona umeweza kumsamehe na moyo
wako bado unamhitaji, hiyo ni ishara ya ukomavu wa kihisia. Kama mkirudiana
pamoja, hakuna tena jambo linaloweza kuwasumbua maana mmepitia mengi.
Ukiona moyo wako bado
unamhitaji hata kama yapo aliyokukosea, tafsiri yake ni kwamba umeona umuhimu
wake na utakapopata nafasi ya kurudiana naye utakuwa makini usimpoteze tena.
Hisia zako zimetulia:
Inapotokea unakorofishana
mara kwa mara na mwenzi wako, zile hisia tamu za mapenzi kati yenu hupotea
kabisa na matokeo yake mnaishi kimazoea. Lakini inapotokea mmetengana na kila
mmoja akaendeleana mambo yake, hisia hutulia na kurudi upya. Mnaporudiana kila
mmoja anakuwa mpya kihisia hivyo mnakuwa na nafasi kubwa ya kudumu.
Hakuna cha kuwayumbisha tena: Ikiwa mmeshapitia kwenye machafuko makubwa yaliyosababisha
mpaka mkaachana, wakati mwingine kwa vurugu kubwa, ni dhahiri kwamba kila mmoja
ameshapata uzoefu.kwani Wahenga wanasema nahodha mzuri wa meli hupimwa wakati
bahari imechafuka.
Hata ikitokea mmekorofishana tena, hakuna
atakayekuwa tayari kuona mnarudi kule mlikotoka hivyo mtamaliza vizuri tofauti
zenu.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv