Related image
Wakati mwingine, inafaa ujipende wewe mwenyewe zaidi ili kufanya mtu mwingine naye akupende. Inafaa uwashe taa fulani ndani yako ili kufungua nishati ambayo inapatikana ndani ya mwili wako ili uweze kuwa mtu tofauti.

Kumfanya mpenzi wako wa zamani kurudiana na wewe si jambo la rahisi kutimiza, haswa kama iwapo ameshachukua hatua ya kusahau yaliyopita na kupata mchumba mpya ambaye wanadate.

Jaribu kuvumbua upande mwingine wa nafsi yako, na ukigundua kuwa unaweza kufanya mambo kama hayo, unaweza kujiamini kufuata maagizo haya ya kutumia saikolojia ili uweze kumfanya mpenzi wako atake kurudiana na wewe.

TUMIA SAIKOLOJIA MJEUKO(JIKAUSHE)

Bila shaka itakuwa wamezoea ya kuwa kila wakati unamfukuzia ama kutaka kujihusisha na kumbabaikia. Lile ambalo utahitaji kufanya ni usijisumbue kumtext wala kumpigia simu.

Kama itatokea mkipishana hata usijisumbue kumuangalia machoni. Akikusalimia mambo wewe mjibu tu poa. Hivi hivi unafaa kuwafanyia marafiki zake. Hakikisha ya kuwa unawafanya kana kwamba huwatambui kabisa katika maisha yako. Wewe jifanye mtu wa kawaida kabisa.

JIPE SHUGHLI KWA KUWA BUZY
Hakikisha kuwa unajipa shughli zako kila muda. Mwanzo kama mnafanya kazi katika jengo moja ama mnasoma darasa moja hakikisha ya kuwa unafanya shughli zako kama kawaida ili uonekane huna muda na mambo ambayo anafanya...yaani humtambui kama yuko hapo.

iwapo itatokea umekuwa na yeye katika sehemu moja jifanye unatext mtu ili mradi usiongee na yeye. Hii itamfanya yeye kujiona mjinga akiwa kando yako sababu wewe upo buzy na shughli nyingine.

USIJIFANYE UONEKANE MWENYE WIVU
Usionekane mwenye wivu. Jiweke asili yako vile ulivyo.
Unaweza fikiria unapishana tu na wapenzi wawili ambayo huwajui kamwe. Usijaribu kuwakimbia.

Ukijaribu kuwahepa utakuwa unatuma ujumbe kwa mpenzi wako wa zamani ukiashiria ya kuwa bado unawapenda na kumwona yeye na mwanamume/mwanamke mwengine kumekufanya uvunjike moyo.

BADILISHA MUONEKANO WAKO. KUWA MTU TOFAUTI
Owk najua ushawahi kuskia zaidi ya mara elfu moja kuwa unafaa kubadilisha muonekano wako ili kujionyesha. Well, kufanya hivi kuna umuhimu gani?
,,, Kujibadilisha kunakupa mwonekano mpya na kunakufanya ujiskia vizuri kuhusu wewe mwenyewe. Kufanya hivi kunakupa confidence na kuweza kujiamini kila mahali utakapokwenda.

,,, Kama unaonekana vizuri, kwa kawaida inakuwa kama ni kioo kinachokumulika ndani yako. Hii itatuma meseji kwa mpenzi wako wa zamani kuashiria kuwa maisha yako hayazunguki kwa mtu mmoja pekee ambaye ni yeye.

,,, Iwapo umejibadilisha kabisa, watagundua ya kuwa kuna nafasi ya haraka kwako kuweza kupata mchumba mwingine. Hii inaweza kumfanya Ex wako kuingiwa na hisia za woga wa kukupoteza asilani. Hivyo kuna uwezekano wa yeye kujipendekeza kwako ili mrudiane.

KUWA MTU USIYEJALI NA UJIBURUDISHE
Tumia muda wako ulionao kuinjoy na marafiki zako. Jumuika na marafiki zako sehemu tofauti, cheka zaidi, enjoy maisha hadi kilele chako.

Iwapo ulikuwa na stress ama mkazo wa maisha wakati ulipokuwa ndani ya mahusiano naye na sahizi umekuwa tofauti itaashiria kuwa umekuwa na utofauti mkubwa na kuwa ndani ya mahusiano naye ilikuwa ni balaa tupu.

JIFUNZE KUKATAA
Ukionyesha kuwa bado unampenda mpenzi wako wa zamani, basi wanaweza kuutumia huu vibaya kwa kuwa hauna uwezo wa kukataa chochote ambacho wanaweza kusema.

Acha kuwa mtu wa aina hii kwa kujikeep buzy na mambo tofauti ya muhimu. Jiheshimu wewe mwenyewe kwa kukataa kutumiwa ovyo. Usikubali kamwe kufanywa mtumwa na mpenzi wako wa zamani. Mwonyeshe kuwa umekuwa tofauti kabisa na mtu ambaye ulikuwa zamani.

INGIA GYM, BORESHA UMBO LAKO
Kuingia gym ni mbinu moja wapo ambayo unaweza kuitumia kusahau mambo yako ya zamani. Pia kuingia gym kunakupa nafasi kwako kujishepu mwili wako ili uwe na toni ya kuvutia. Pia gym inakusaidia kukupa confidence na kujiamini. Pia gym inakufanya uwe na nguvu zaidi.

ACHA/PUNGUZA KUMSIFIA

Mjibu kwa kumsifia lakini usiingie sana. Unaweza kumwambia "Pia wewe umependeza lakini mtindo wa nywele zako umekaa vibaya na nguo" ama "Hio nguo uliyovaa inaweza kufanya kila mwanamke akuangalie lakini marashi uliopaka yananuka vibaya"

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top