Kwanza kakakuona Ndiye mnyama pekee duniani ambaye mwili
wake wote umefunikwa na
magamba makubwa Magamba yanayofunika mwili wa mnyama huyo ni makubwa kuliko ya viumbe wengine na magamba hayo kitaalamu yameundwa na kitu ninachoitwa ‘keratin’, ambayo yanafanana na yale yanayounda kucha za binadamu na Asilimia 20 ya uzito wa mwili wa mnyama huyo unatokana na magamba.
magamba makubwa Magamba yanayofunika mwili wa mnyama huyo ni makubwa kuliko ya viumbe wengine na magamba hayo kitaalamu yameundwa na kitu ninachoitwa ‘keratin’, ambayo yanafanana na yale yanayounda kucha za binadamu na Asilimia 20 ya uzito wa mwili wa mnyama huyo unatokana na magamba.
Kakakuona hutumia magamba hayo kama silaha ya kujilinda
dhidi ya maadui.
Maana ya jina hilo la kakakuona ilianzia nchini Malaysia, Indonesia na Brunei
likimaanisha kitu kinachojikunja.
Kakakuona hupenda kujikunja kama mpira. Hiyo ikiwa kama
mbinu anayotumia kujilinda dhidi ya maadui. Licha ya kuwa hutumia mbinu hiyo
kujilinda, lakini anapojikunja ndiyo inakuwa rahisi kwa watu kumkamata na
kumbeba.
Huishi juu ya miti na
katika mashimo
Baadhi ya kakakuona huishi juu ya miti, wengine hujichimbia
ardhini na kuishi ndani ya mashimo.
Wengi wanaoishi juu ya miti ni wale wenye mikia mirefu
wanaopatikana barani Afrika. Wengine huchimba mashimo marefu ardhini na kuishi
humo ili wasikutane na binadamu.
Si rahisi kushambuliwa
na wanyama wengine
Ukiachilia mbali adui yao mkubwa ambaye ni binadamu, adui
wengine wa wanyama huyo ni jamii ya chui na simba.
Hata hivyo, maadui hao hushindwa kuwashambulia kakakuona
kutokana na namna wanavyojilinda kwa kujikunja na jinsi mwili wao ulivyo na
magamba.
Kutokana na hali, hiyo inakuwa vigumu kwa simba au wanyama
wengine kuwashambulia kwa kuwala. Hakuna anayefahamu idadi ya miaka anayoishi
Inakadiriwa kuwa mnyama huyo huishi kwa kipindi cha miaka 20 akiwa katika pori.
Lakini hiyo ilikuwa inafahamika zamani kipindi ambacho mnyama huyo alikuwa
anaonekana tofauti na sasa.
Hata hivyo, kutokana na aina ya maisha ya wanayoishi,
inasemekana kuwa wanaweza wasiishi miaka mingi, licha ya kuwa bado haifahamiki
kwa sasa, inawezekana wakaishi kwa miaka 20. Hutema sumu kali mithili ya
tindikali Kakakuona akiona adui hujilinda kwa kujikunja, lakini akiona hali
inakuwa mbaya zaidi, hutema sumu kali mithili ya tindikali inayoweza kumdhuru
adui.
Pia, wakati mwingine hunyoosha mkia wake na kuuzungisha na
kumkata adui aliyekaribu yake.
katika miaka 10 iliyopita Inakadiriwa kuwa kakakuona 100,000
hukamatwa kila mwaka barani Afrika na Ulaya na kuuzwa.
China na Vietnam ndizo nchi maarufu ambazo nyama na magamba
yake huuzwa. Kutokana na hilo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Hifadhi za Asili
(IUCN) limemweka kakakuona kwenye orodha ya wanyama walioko kwenye hatari ya
kutoweka duniani.
Hawaoni vizuri Ni aina moja katika ya nane za kakakuona
wenye uwezo wa kuona vizuri hasa muda wa mchana. Hawa ni wale wanaopatikana
barani Afrika.
Wengine hawana uwezo wa kuona vizuri kutokana na kuwa na
macho madogo.
Lakini Wana uwezo mkubwa wa kunusa na kusikia Licha ya
wengine kuwa na macho madogo na kushindwa kuona vizuri, kakakuona ni mnyama
mwenye uwezo mkubwa wa kusikia sauti yoyote kwa haraka kwa sababu masikio yake
yameinuka. Pia, ana uwezo mkubwa wa kunusa harufu yoyote.
Ni vigumu kujamiiana
Tofauti ilivyo kwa baadhi ya wanyamaa, upande wa kakakuona
tendo kujamiiana ni gumu kutokana na tofauti za kimwili kati ya jike na dume.
Mwili wa kakakuona dume una uzito mkubwa zaidi ya asilimia 50 ukilinganishwa na
jike. Mbali na hivyo, hawana msimu maalumu kukutana na kujamiiana, tofauti na
ilivyo kwa wanyama wengine.
Uhusiano na wanyama
wengine
Imezoeleka kuwa, mnyama huyo huwa karibu na wanyama wengine
wa jamii yao, kwa maana ya wale wanaokula wadudu.
Hata hivyo, hivi karibuni wanasayansi wamebainisha kuwa
wamekuwa karibu na wanyama kutoka jamii nyingine kama wale wanaokula nyama.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv