kitendo cha mtu kubanwa na haja ndogo siyo
kitu cha hiyari kwamba sasa mtu anaamua ngoja nibanwe na mkojo, hili ni jambo
la asili na ni matokeo ya vyakula, matunda au vinywaji tunavyotumia. Kwa lugha
nyingine tumekuwa tukiita kuwa ni wito wa asili au nature’s call.
Uenda mtu ukawa, safarini, ukawa katika
mitandao ya kijamii unachati au popote pale akiwa anafanya jambo fulani na
kutokana na jambo hilo, mtu akaendelea kujibana na kutokwenda kuyapunguza maji
haya kutoka katika kibofu cha mkojo kwa kutoa kipaumbele kwa shughuli
anayoifanya kuliko kusikiliza kwanza wito huu wa asili.
Mambo haya tunayafanya sana, utasikia, mkojo
umenibana kweli, ila ngoja nimalizie hii kazi halafu niende kujisaidia, hivi
ndivyo watu wengi wanafanya.
Kwa kawaida kibofu cha mkojo huanza kujaa
mkojo, unapofikia karibu mililita 50 mpaka 500 mtu huanza kuhisi hitaji la
kwenda kukojoa.
Kibofu cha mkojo kimezungukwa na vigunduzi
asili yaan (Receptors) vinavyopeleka taarifa katika Ubongo kuonyesha kuwa kibofu
cha mkojo kimekaribia au kimejaa, na baada ya taarifa hizi kufika katika
ubongo, ubongo unatoa taarifa katika kibofu cha mkojo ili kiweze kushikilia
mkojo huo kwa kuikaza misuli maalumu mpaka hapo muda wa wewe kwenda kukojoa
utakapofika.
Kibofu cha mkojo hufanya kazi kwa mfumo wa
kujiendesha wenyewe yaani, automatic, kwa hiyo kitendo cha mtu kupuuzia kwenda
kukojoa husababisha Ubongo upate usumbufu wa taarifa za kujaa kwa kibofu cha
mkojo na kwa kuwa Ubongo nao hutuma taarifa katika kibofu cha mkojo kusema kuwa
mkojo uendelee kushikiliwa mpaka muda muafaka utakapofika, itafika kipindi
uwezo wa ubongo kutoa taarifa hizi na pia uwezo wa vigunduzi asili
yaan (Receptors) vilivyoko katika kibofu cha mkojo kupoteza uwezo
wake tena wa kufanya kazi hizo au uwezo kuwa mdogo.
Matokeo yake ni mtu siku kweli anahitajika
kuvumilia kidogo ili afike sehemu inayostahihi kujisaidia, lakini hawezi tena
na kujikuta muda mdogo tu.
Kwa hiyo mtu kujibana na kupuuzia
kwenda kukojoa husababisha uwezo wa kibofu cha mkojo kujitawala (control)
upotee.
Pia kama uwezo wa neva zinazopeleka taarifa
kwenye ubongo kuhusu mabadiliko/ujazo wa kibofu cha mkojo zitaharibika, basi
misuli maalumu ya kubana mkojo itashindwa kuachia na matokeo yake mtu
ataendelea kukaa na mkojo katika kibofu chake kwa muda mwingi zaidi kitu
ambacho ni hatari kwa afya yako.
Endapo mkojo huu utashindwa kutoka,
utatengeneza mazalia ya bakteria na kukusababishia magonjwa ya kibofu (bladder
infection). Magonjwa ya kibofu cha mkojo ni pamoja na U.T.I (Urinary Tract
Infections), pia huweza kusababisha magonjwa ya figo na mchafuko wa damu,
bacteremia.
Kuna hali huwa inajitokeza kwa baadhi ya watu,
yawezekana alikuwa kabanwa na mkojo au alikuwa hajahisi kwenda kukojoa, ila
akinywa maji au akisikia sauti ya maji yanachuluzika mfano maji yakitoka
bombani, basi atahisi kwenda kukojoa.
Aweza kuwa matatizo yatokanayo na kubana mkojo
kwa muda mrefu
Ni vyema na ni vizuri tukawa
wasikivu unapobanwa na mkojo, hii ni kwa ajili ya afya ya kibofu chako cha
mkojo lakini pia ni kwa ajili ya afya yako kwa ujumla. Kama unalo tatizo,
usisite kuonana na wataalamu wa afya Watakusaidi
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog
na youtube@edone tv