NA MARTHA MAGAWA
Watu hupigana,
watu huachana, hujeruhiana, hutukanana na hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata
hivyo, si wote wanaojua wafanye nini wanapoingia kwenye hatua hiyo mbaya. hebu
jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana
jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura
kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine
mkaamua kuachana.
1. MPUNGUZE MHEMKO
Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu
aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa
jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokeo yajayo badala yake
hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi, iwe kwa maneno au kwa
mapambano.
Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka
kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Jambo la muhimu hapo ni
kuacha kumwandama, kujibizana naye au kumshawishi akusikilize. Badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake.
2. MSOME SAIKOLOJIA YAKE
Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina, itakuwa rahisi kwako
kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya
kawaida. Ukilifahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikolojia ili
kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka
kumwambia wakati alipokuwa na hasira.
Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku
mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za
mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi.
3. MRUHUSU AKUJIBU
Pamoja na kumsoma kisaikolojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea. Mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha.
4. EPUKA MALUMBANO
Kama nilivyosema hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kuhamaki tena.
5. MUOMBE MSAMAHA
Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri,
usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kuzungumza ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv