Image result for upendo
NA. MARTHA MAGAWA

Kitu kinachowasumbua wengi, anataka akimpenda mwenzi wake na
kumuonesha mapenzi ya dhati na yeye arudishiwe mapenzi vilevile kama yeye anavyotoa.

Hata hivyo, siyo sahihi kutegemea mwenzi wako naye akupende kama unavyompenda. Badala ya kukaa kusubiri kuona naye anakurudishia mapenzi ya dhati kama unayompa, unachotakiwa kufanya ni kujipenda wewe kama unavyompenda yeye, au pengine hata zaidi ya hapo.

Upendo una kawaida ya kuvutana, yaani mtu anayejipenda ni rahisi sana kupata mtu ambaye atampenda kwa moyo wake wote.

Upendo huwa haujifichi, kwa maana mtu anayejipenda huwa ni rahisi sana kumtambua na hata mtu asiyejipenda pia ni rahisi kumgundua kwa
kumtazama tu. Hutakiwi kujikatia tamaa, kama kwa kipindi kirefu
ulikuwa huoni umuhimu wa kujipenda, anza leo.
Image result for upendo
Hakikisha muda wote unajifanyia mambo mazuri wewe kwanza, baada ya hapo ndiyo umfikirie mwenzi wako. Kama unajipenda, hata ikitokea
mwenzi wako akawa hakuoneshi mapenzi kama unayompa, au akakutenda, bado utakuwa na ujasiri mkubwa wa kusonga mbele kwenye maisha yako bila kutetereka.

Wanawake, wengi wanapokuwa kwenye hatua ya kulea watoto wadogo, huwa wanajisahau sana katika suala zima la kujipenda na kuelekeza nguvu na akili zote kwa watoto.

Hawakumbuki tena kujipamba na kupendeza wala kuwa na mwonekano utakaowafanya wenzi wao waendelee kutamani kuwa nao karibu.

Hata kama unanyonyesha, jipende na jithamini, ukizingatia
haya, mateso ya kimapenzi utakuwa unayasikia kwa wenzako tu.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top