MARTHA MAGAWA
Watu wengi wako kwenye uhusiano wa kimapenzi bila kujua kama kweli wanapenda kwa dhati au wanajilazimisha sasa Ili kutambua upendo wako jipime kwa maswali yafuatayo: Unapoamka asubuhi wazo la kwanza kukujia linamhusu mpenzi wako au unafikiria zaidi kazi na mambo mengine? Una msukumo wa kutaka kumsalimia na pengine kumuuliza anapenda afungue kinywa kwa chakula gani? Je umekuwa mwepesi na mwenye furaha kubwa kuwaambia rafiki zako wa karibu juu ya hisia zako kwa mpenzi wako? Unajisikiaje wanapokushawishi vibaya kuhusu yeye? Je, anapokwambia anakuja kukutembelea huwa unajisikia hamasa moyoni kiasi cha mwili kusisimka? Unapokuwa peke yako mawazo yako yanatawaliwa na yeye au unafikiria kucheza gemu kwenye simu yako na kujifariji kwa vitu vingine? Unapompima kwa kumlinganisha na wengine anachukua nafasi ya kwanza au anazidiwa? Je, unapomfikiria na kupata kivutio fulani ndani ya moyo wako kuhusu ucheshi na utani wake huwa unatabasamu hata ukiwa peke yako? Unajisikiaje wazo la kusalitiwa linapokujia, unaona ni sawa au unahuzunika kiasi cha kupoteza furaha na kutamani uambatane naye kila aendako ili usiibiwe? Hebu jiulize ni mara ngapi umekuwa ukishawishika kumnunulia mpenzi wako nguo, mapambo au vitu kwa lengo la kumfanya avutie au ndiyo umemtelekeza na kumwacha aonekane mchafu na asiyevutia mbele za watu? |
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv