Tunapokuja
katika suala la mahusiano mazuri lazima Wewe
kijana au mwanaume ujue kuna mambo mhimu ambayo uantakiwa kuwa nayo ili kumpata
umpendae unatakiwa kujua nini cha kufanya
kwa ajili ya kulifanya penzi lako lizidi kuchanua na kuwa jipya kila kuchapo.
KUJIAMINI
Mwanamke
anajisikia salama zaidi akiwa na mwanaume ambaye anajiamini – mwenye uwezo wa
kutetea hoja zake na kujieleza sawia. Siyo anayebabaika. Wakati mwingine,
mwanamke anaweza kukupima hata katika jambo ambalo amekosea yeye, ataangalia
unavyotoa maamuzi yako na, atafuatilia kuona kama utakuwa mwepesi wa
kuyabadilisha maamuzi yako.
KUJALI
Wanawake
wanapenda sana wanaume wanaojali Kama huna tabia hiyo, ujue upo katika nafasi
kubwa ya kumkwaza mpenzi wako. Mjali mpenzi wako kwa kila hali. taka kujua
maendeleo yake,mpe nafasi kubwa sana ya
kuendelea kudumu katika uhusiano hai.
USAFI BINAFSI
Asilimia
kubwa ya wanawake wanapenda sana usafi. Mwanamke anavutiwa sana na mwanaume
mtanashati. Usafi wako unamfanya ajiamini kuwa na wewe.
KUJITETEA
Wakati
unapodai haki yako mbele ya mwanamke wako, suala la kujitetea linapewa nafasi
kubwa sana.
Wanawake
hawapendi kuwa na wanaume ambao wapo tayari kuonewa. Wanataka wenye uwezo wa
kusimama kidete kuona haki zao hazichukuliwi kirahisi.
UKARIBU
Hapa
namaanisha kuwa naye katika mambo mengi
unayoyafanya kila siku. Ni vizuri kuwasiliana naye mchana, ukitaka kujua aina
ya chakula alichokula siku hiyo au ikiwezekana mchagulie na mambo mengine kama
hayo.
KUMSIFIA
Usipuuzie
hili Hali ni tofauti sana kwa wanawake
ambao hupenda kuwasifia wanaume zao. Msifie mkpenzi wako tu kwa zile sifa alizo
nazo usuzidishe na za uongo.
MALENGO
Wanaume
wengi hawapendi kuwashirikisha wanawake katika mambo yao. Usifanye mabo yako
kwa siri bila kumshirikisha mwenza wako mshirikishe katika malengo yako na kile
unachofanya.
KIPAUMBELE
Mpe
mpenzi wako kipaumbele katika mambo tofauti tofauti unayokuwa unafanya
muonyeshe kuwa yeye n wa maana na mhimu katika maisha yako.
TENDO LA NDOA
Hakika
hili ni jambo nyeti, kinachohitaji lugha
nzuri ya kirafiki kukifafanua. Hakuna siri, tendo la ndoa ni moja ya kiwakilishi
cha ndoa. Kimsingi tendo la ndoa lina nafasi yake. Ni muhimu likaheshimiwa na
kutengewa muda maalum wa kufurahia. Acha papara kabisa.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz ,twiter@edonetz ,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv