Oga maji ya baridi, Hii inasaidia kuimarisha afya ya mwili na akili pia inaleta mabadiliko ya kudumu kwenye mfumo wa kinga ya mwili na ubongo.
Mazoezi ya viungo Ili uwe miongoni mwa watu wenye afya bora, furaha na kiwango kikubwa cha uzalishaji duniani, jiwekee mazoea ya kufanya mazoezi mara kwa mara. sio mpaka uende gym na kunyanyua vitu vizito, fanya mazoezi ya kawaida tu itakusaidia.
Kula angalau gramu 30 za protini Vyakula vyenye protini nyingi vinafanya ushibe muda mrefu zaidi ya vyakula vingine kwa sababu vinasagwa kwa muda mrefu zaidi. Pia, protini inasaidia kuweka kiwango cha sukari kwenye uwiano mmoja, vyakula hivyo ni pamoja na mayai, maziwa, mboga mboga na mazao kama karanga, korosho nk.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz ,twiter@edonetz ,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv