Jifunze kushukuru. Hakikisha Kila siku ukiamka asubuhi Mshukuru Mungu. Kitendo hicho kitakufanya ujione una jambo la kushukuru na kuwa wewe ni mwenye bahati. Fikiria mambo matano ya kushukuru kila siku asubuhi na utajiongezea furaha maishani mwako.
Jiwekee utaratibu wa kuamka mapema, Uchunguzi unaoyesha kuwa watu wanaoamka mapema wanakuwa na furaha zaidi kuliko watu wanaochelewa kuamka. hivyo basi jitahidi kuamka mapema na kuamka mapema kunakufanya uanze siku yako vizuri.
Jitahidi kupanga ratiba ya siku nzima, kuna wakati unaweze kuwa umefanya kazi nyingi lakini ukiangalia unaona kama hakuna ulichokifanya, Hii inasababishwa na ktokuwa na ratiba nzuri inayoeleweka hakikisha unaandika list ya vitu unavyopanga kufanya kwa siku nzima, mwisho wa siku ukija kuangalia utaona hatua za kile ulichokifanya , utajipongeza na kulala vizuri ukijua siku yako imekuwa ya mafanikio.
Tenga muda wa kufanya kitu unachokipenda , mfano kuangalia movie, kusikiliza muziki, kuangalia mpira, kujumuika na wenzako, kuendesha gari nk.
Wafanyie watu mambo mema, Hii itakufurahisha wewe na ambaye umemfanyia jambo jema, Mambo ya kufanya kumfurahisha mtu ni mengi sana katika jamii , Hakikisha kila siku unamfanyia mtu jambo jema na itakuongezea baraka na uwe na furaha siku zote.
Mpigia simu mtu umpendae na umwelezee hisia zako za moyoni jitahidi kusema neno nakupenda na kuelezea hisia zako moja kwa moja kwa mtu umpendaye bila kuficha, yawezekana ukawa uanaongea na mke wako , mtoto wako au mtu wako wa karibu. Kuna miujiza katika neno nakupenda na kuonyesha hisia wazi , ukilitumia vizuri utaiona hiyo miujiza.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz ,twiter@edonetz ,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv