MUONYESHE HESHIMA NA SHUKRANI
jifunze kuwa na shukrani hata kwa mambo madogo anayokufanyia, Hata kama ame kununulia pipi, au kama mwenzi wako amekupa zawadi au kitu ambacho hujakipenda, muonyesha shukrani kwanza alafu ndio umuonyeshe hujakipenda.
KUWA NA MUDA WA KUMCHUNGUZA NA KUMUELEWA
Unatakiwa umchunguze akiwa na hasira anakuwaje na akiwa na furaha anakuwaje, anapenda sana kufanya mambo gani (hobi) au anapenda sana zawadi za namna gani. Ukishamjua, ni rahisi sana kuishi naye hata pale anapokasirika au anapokerwa na jambo fulani.
Jishushe na kuwa na utaratibu wa kumuomba msamaha unapokosea ila usiombe msamaha kama hujakosea, Bila kujali kwamba wewe ni mwanaume au mwanamke, mkubwa au mdogo, una fedha au huna, inapotokea umeziumiza hisia za mwenzio,ni lazima uombe msamaha na kuahidi kutorudia makosa.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz ,twiter@edonetz ,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv