Funza wa vitumba (American bollworm) ni mabuu (larva) ya mdudu jamii ya kipepeo ambayo hushambulia mmea ,ni muhimu kubaini funza kabla hajatoboa matunda.
Funza wachanga hula majani baadae matunda, wakishaingia ndani ya matunda husababisha uharibifu mkubwa na kusababisha matunda machanga kupukutika na matunda yaliokomaa husababisha matundu ambayo huruhusu kuingia na kuenea kwa magonjwa kama ukungu na bacteria.
Cha kufanya.
Hakikisha unakagua mazao mara kwa mara ili kumbaini mdudu ;
Angalia majani yaliyo chini ya maua ya juu yaliochanua kwa kutafuta mayai ya viwavi.
Jinsi ya kuzuia;
Ondoa na teketeza matunda yalioathirika ,
Toa funza kwa mkono na teketeza mayai na funza wadogo wadogo ,
Epuka kupanda nyanya karibu na pamba au mahindi.
Ondoa na teketeza mabaki baada ya kuvuna.
Tumia dawa ya kuua waddudu.