Taasisi tisa za
serikali ikiwamo Taasisi ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) na
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, zimetajwa kuwa na viashiria vya rushwa.
Hayo yameelezwa leo na
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Matern
Lumbanga.
Maeneo matano
yaliyoangaliwa ni ukidhi wa sheria ya manunuzi ya umma, ukiukwaji wa sheria na
taratibu za manunuzi, kupima thamani halisi ya fedha ilivyotumika, malipo yenye
utata na viashiria vya rushwa.
Hatua hiyo ni matokeo
ya ripoti ya ukaguzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma(PPRA) ,
iliyofanya ukaguzi wa manunuzi ya umma katika kipindi cha mwaka 2015/16 huku
ikihakiki ukaguzi wa ukaguzi iliyofanya 2014/15.
Kwa mujibu wa ripoti
hiyo, PPRA ilikagua Taasisi 70 kati ya 104 iliyopanga kukagua, mikataba 21,313
ya manunuzi yenye thamani ya Sh. 1.05trilion ilikaguliwa.Jumla ya Taasisi
nchini ni 493.
Source: Mwananchi