Kundi moja la wataalam nchini China limeshinda tuzo
la shindano la kuonja mvinyo nchini Ufaransa.
Watalaam
hao walitambua mivinyo waliopewa huku wakiwa wamefunikwa uso,wakibainisha
asili, aina ya zabibu zilizotumika na mwaka mivinyo hiyo iliotengezwa.
Waandalizi
wa shindano hilo waliwataja wataalam hao wa China kuwa mabingwa katika
ulimwengu wa mvinyo.
Waliyashinda
mataifa mengine 20,ikiwemo washindi wa awali Ubelgiji na Uhispania.
Huku mapato yakiongezeka
nchini China,taifa hilo linaongoza katika utengezaji na utumiaji wa mvinyo
duniani