Uwezo wa ubongo wa binadamu katika kutunza kumbukumbu ni wa hali ya juu. Ubongo una neurons karibu bilioni moja na kila neuron inaunda njia takribani elfu moja zinazounga neurons
nyingine hivyo kuleta miunganiko zaidi ya trillioni moja. Laiti kama kila neuron ingekuwa inatunza kumbukumbu moja basi tungesema basi ubongo limit yake ya kutunza kumbukumbu ni pale zinapokaribia bilioni moja, lakini sivyo.

Miunganiko hii ya neurons inatengezeza mtandao mkubwa sana wa kupokezana kumbukumbu kwa wakati mmoja na hivyo kufanya uwezo wa kutunza kumbukumbu hizi uwe mkubwa sana kiasi kwamba hauwezi kujaa katika maisha yote ya binadamu hata akiishi miaka mia moja. Hii pia ni kwa sababu neurons katika ubongo zinaendelea kukua katika maisha yote ya binadamu.

Kwa kulinganisha na utunzaji wa kumbukumbu katika computer, uwezo wa ubongo ni sawa na 2.5 petabytes au one million gigabytes. Vifaa vyote tunavyoviona kama latest technological devices kama smart phones, ipads, PCs, GPS devices na vinginevyo vina uwezo wa chini sana wa kutunza kumbukumbu kama vikilinganishwa na ubongo wa mwanadamu. Lakini pia kuna super computers kama K-Fujitsu hii ni exceptional kwa kutunza kumbukumbu ubongo wa binadamu hausogei (sio ufanyaji kazi)


Lakini mbona tunasahau? 

Kusahau kule kwa kawaida ni jambo la kawaida la binadamu na lina sababu zake na labda pia umuhimu wake. Kujifunza kwa nini ubongo huruhusu kusahau sio kitu kidogo bali hili ni eneo pana sana la psychology na lina wataalam waliobobea kutambua kwa nini tunasahau.

Kuna theories zake zinazoelezea jambo hili la ajabu la ubongo na zenye nguvu zaidi ni ile ya kufutika kwa kumbukumbu za muda mfupi (Trace decay and displacement) na ile ya kufutika kwa kwa kumbukumbu za muda mrefu. (Interference and lack of consolodation)

Kwa theory ya kwanza (trace decay theory) inaelezea kumbukumbu ina kawaida ya kuacha alama(trace) katika ubongo. Hapa trace inakuwa kwa maana ya mabadiliko fulani ya kikemia au kifizikia ndani ya mishipa ya ufahamu.

Sasa kinachotokea ni kwamba kusahau kunakuja kama matokeo ya asili ya kufutika au kufifia kwa hizi alama za kumbukumbu zilizoachwa. theory hii inapendekeza kuwa kumbukumbu za muda mfupi hutunzwa kwa muda wa sekunde 15 hadi 20 na kama hazikushughulikiwa basi hupotea au kufutika. Utafiti uliofanywa zamani sana na unaojulikana kama Brown-Peterson task unasapoti hii theory.

Theory ya pili (interference and lack of consolidation), hii inapendekeza kuwa baadhi ya kumbukumbu hupambana na kuingiliana ili kupata nafasi katika sehemu zinapotunzwa. Kama kumbukumbuku ya iliyotunzwa mwanzo inafanana na nyingine inayoingia basi kuingiliana kwa kumbukumbu hizi ni dhahiri.

Inaweza kutokea kwamba kumbukumbu iliyotunzwa kabla ina nguvu zaidi na inazuia kumbukumbu mpya isitunzwe (Proactive interference) na pia inaweza kutokea kumbukumbu mpya haipati nafasi kwa kuwa uwezo binafsi wa mtunza kumbukumbu hauwezi kustahimili kumbukumbu mpya.

Vipande vingine vinavyojenga theory ya kwanza na hii ya pili ambayo hasa ni kushindwa kukumbuka au kuvuta kumbukumbu ni kama "Generic cues" pale ambapo mzizi wa kumbukumbu unafanana. "Repression" pale ambapo kumbukumbu inafanyiwa makusudi ifutike pale ambapo kumbukumbu hii ina madhara. Pia hali ya ubongo inaweza kusababisha kupotea kwa kumbumbuku hii ni kutokana na magonwa mbalimbali kama Amnesia, Jipu la ubongoni (Brain tumour) na mengineyo.

Mambo mengine tofauti na utunzaji wa kumbukumbu

Fahamu (neuron impulses) kwenda na kutoka katika ubongo husafiri speed ya kilomita 270 kwa saa. Huu ni mwendo mkali sana ukizingatia kutoka kwenye kidole cha mguu wako kwenda kwenye ubongo ni kama sentimita 160 tu. Lakini kuna aina tofauti za neurons na hivyo speed inatofauitiana katika kila aina baadhi speed hupungua hadi nusu mita kwa sekunde (0.5 meters/sec) au kuongezeka sana hadi mita 120 kwa sekunde (120 meters/sec).

Nishati inayotengenezwa na ubongo wa binadamu ni sawa na ile ya kuwasha balbu ya wati kumi (10 watts). Hii ni hata ukiwa umelala. Hivyo kwa kipindi kirefu cha maisha chukulia taa hii ya watt 10 inawaka. Na ubongo huwa active zaidi pale mtu anapolala tofauti na wengi wanavyodhani kwamba tunapolala basi ubongo hupumzika.

Katika vipimo vya nguvu inayotumika wakati wa mchana ukiwa kazini na majukumu ya kawaida au hata ukiwa unafanya hesabu ngumu bado ni ndogo ikilinganishwa na ile inayotumika ukiwa umelala unaota. Na inasemekana wale watu wenye I.Q kubwa kuwa wanaota ndoto sana kulinganisha na wale wenye I.Q. ndogo.

Binadamu anaota ndoto zaidi ya elfu katika usiku mmoja ila kwa kuwa nyingi ni fupi sana hivyo hazitunzwi katika ubongo na unapoamka huwezi kukumbuka. Hii kitu bado inasumbua vichwa vya wataalamu wa mambo ya ubongo.

Jambo jingine kubwa la uwezo wa ubongo wa binadamu ni kubeba information nyingi sana kwa wakati mmoja. Information hizi zinatokana katika milango yote ya fahamu na zinaweza kuchambuliwa kutafsiriwa, kupangwa, kuitikiwa na kutunzwa kwa wakati mmoja.

Seli mpja ya ubongo wa binadamu ina uwezo wa kushikilia information sawa na kitabu kimoja kizima cha Encyclopedia. Encyclopedia ni kitabu kama kamusi ya tawi la elimu fulani. Encyclopedia ya utamaduni basi itakuwa na summary ya kila kitu kuhusu utamaduni kwa mpangilio wa mfuatano wa herufi (a-z).

Viumbe wengine wenye kumbukumbu kubwa

Kuna baadhi ya viumbe wenye uwezo fulani mkubwa sana katika bongo zao lakini bado hakuna aliyethibitishwa kumzidi mwanadamu.


Ndege wa aina nyingi wana uwezo fulani wa kumbukumbu (spatial memory) ambao huwasaidia kuishi katika mazingira magumu. Mfano njiwa wale wanaoishi mijini wana uwezo wa kukumbuka sura ya binadamu katika details za kushangaza. Ukimtisha njiwa mmoja akakuona vizuri zura yako ukirudi baada ya wiki hata kama umebadili nguo na unatabasamu yule njiwa atakutambua na kuruka mbali haraka. Hivyo hivyo ukimpa chakula na kuonesha huna hatari kwake akikuona sura vizuri hata ukirudi baada ya mwezi njiwa yule atakukumbuka na kuruka karibu yako. Hii ni kwa sababu ubongo wake hutunza kumbukumbu za tabia fulani za uso ambazo zimetofautiana kati ya kila binadamu. Pia kuna sokwe mtu hawa wanajulikana kwa kumbukumbu za aina mbalimbali ikiwemo visual memories.


Wengine ni Sea lion na Tembo, hawa wana kumbuka vizuri sana pale wanapooneshwa kitu alafu kujaribiwa kama watakumbuka hata katika hali ya kuchanganywa sana. Tembo huweza kutambua kundi lake hata likiwa na tembo wengine mia na hamsini atawakumbuka wote. Na pia wengine waonaingia katika list ya uwezo wa hali ya juu wa kukumbuka ni pweza na paka. Ubongo wa pweza hufanya kazi kama ubongo wa binadamu na si viumbe wenzie wa majini. Pweza pia anauwezo wa kutunza kumbukumbu ndefu na fupi na hweza kuziunga katika hali fulani ya hatari hivyo kufanya mambo ambayo hata binadamu angehitaji muda zaidi wa kufanyia mazoezi. Paka huyu tunaishi nae majumbani mwetu na labda tunamdharau tu lakini ni kiumbe mwenye kumbukumbu kali za muda mfupi ambazo zake ni ndefu kuliko za binadamu.


 
Top