Ukiachana na kunyanyua
vyuma vizito, zipo njia nyingine za kukuza misuli na kufanya mwili kuwa katika
hali ya mvuto kuliko hata ya myanyua vyuma, na kuufanya mwili kujijenga kwa
usawa bila kuwa na utofauti wa ukubwa wa misuli ambao wanyanyua vyuma vizito
wengi wao walivyo, haya hapa ni mazoezi kumi na matano yatakayokuweka vizuri
kiafya na kimuonekano...
kama zifuatavyo..
·
Push
up
Ni zoezi linalopanua kifua, kujenga
kifua, kukuza misuli ya mikono ya ndani na nje na ni zoezi zuri la kuanzia,
kama unataka kuwa na mwili wa kujijenga vizuri anza na hili zoezi.
·
Pull
ups
Pull ups inafanyisha kazi kila misuli mwilini,
hasa misuli ya mikono na mgongo, ukitaka uwe na nundu za mikono kama za Jean
Claud Vandame hili ndo hasa zoezi lako.
·
Plank
Ukishikilia hili zoezi
bila kutingishika kwa dakika kadhaa, wewe kweli utakua una nia na kuubadilisha
mwili wako liwe hekalu la mvuto. Zoezi hili linahitaji mabega yaliyoshiba na
linafanyisha kazi misuli ya mikono, kiuno, mgongo, shingo na miguu na zoezi hili
lina zawadi moja, linafanya tumbo lako likatike mara sita.
·
Roll
Out
Hili zoezi linafanana
na la nusu push up(Plank), ila linachobadilisha ni kusukuma nondo kuelekea
mbele na kurudi, na jinsi unavyoendelea kusukuma nondo ndo ambavyo zoezi
linavyozidi kuwa gumu, kwa hio unahitaji nia na kujitoa kweli, faida zake
linajenga misuli ya mgongo, kiuno, kifua na kutanua mabega.
·
Glute
bridge
Zoezi hili linajenga
mgongo na misuli yote inaouzunguka, ukiwa mkufunzi wa hili zoezi kinachofuata
ni kuombwa namba tu na wasichana.
·
Iverted
Row
Hili zoezi ni la
mgongo, fuata kama picha inavyolionyesha, faida zake linafanya kifua kiwe
kipana zaidi na mikono iwe na stamina zaidi.
·
Close
Hands Push ups
Hili zoezi ni kwa
ajili ya mikono, na ni kwa ajili ya nundu za ndani na nje ya mikono, na misuli
yako inakua inakua kwa pamoja bila kutegeana, fanya hili zoezi na utaona
mabadiliko makubwa kwenye mikono yako.
·
Star
Plack
Hili zoezi kidogo ni
zito kidogo, na zoezi hili linalenga kifua na mabega pamoja na misuli ya miguu
na mikono, na ni zuri kwa kukata tumbo.
·
Burpee
Zoezi la kupunguza
mafuta mwilini, zoezi hili linafanya mwili mzima uchemke kwa pamoja, ukiwa
unafanya hili, unakua unafanyisha kazi kila kiungo cha mwili na kuondoa sehemu
dhaifu mwilini.
·
Dip
Zoezi la misuli ya
nyuma ya mkono na linasaidia pia kwenye misui ya kifua na upanuaji wa mabega na
kufanya kifua kikae vizuri, zoezi hili linahitaji nia na nguvu ili lifanyike
kwa mpangilio unaotakiwa na linamzidi yule aliyelala kwenye benchi akinyanyua
vyuma vizito.
·
Bulgaria
Split Squart
Kichura chura cha mguu
mmoja nyuma, kinafanyisha kazi misuli ya mapajani na kukufanya uwe na stamina
zaidi, ukifanya hili kwa wiki kadhaa, kama kichura chura cha kawaida kilikua
kinakupiga chenga basi utakua unafanya mara mbili ya zaidi ulivyokua unafanya.
·
Suspended
Push ups
Push ups ni nzuri, ila ukiiongezea ugumu
kidogo kwa kuiongezea suspenda, ni njia mojawapo ya kuiongezea misuli uzito, na
kufanya iwe misuli yenye ujazo na ya muda mrefu tofauti na yule anaebeba vyuma
vizito.
·
Prone
Back Extension
Hili zoezi
linahimalisha kiuno, tumbo na mgongo kwa ujumla.
·
Pike
Push ups
Ukiwa mkongwe wa push
ups, hili ndilo zoezi la mwisho la push ups na linasaidia kuimalisha mabega na
kuongeza ubora wa viazi vyako vya mikono.
·
Swiss
Ball Rollout
Zoezi linavyozidi kuwa
gumu ndo misuli inavyozidi kuongezeka, ukiweza kuzingatia haya mazoezi
utajishangaa baada ya wiki tatu mfululizo ukiwa unayafanya.
ahsante sana @mtumkubwa endelea kushirikiana nami na kunisapot karibu