hizi hapa aina za maumboya na mavazi yatakayokufaa ila  Jambo muhimu ni kujua vipimo vyako ili ujue unaingia kundi lipi. karibu..

Kundi la Apple


Umbo la namna hii na mabega mapana, vipimo vya kifua havitofautiani sana na kiuno, ana kifua kikubwa, mkubwa tumboni na miguu mirefu isiyokuwa minene sana.
Iwapo upo kundi hili, chagua nguo zinazoshape lakini zisizobana mwili, Chagua zenye nafasi kifuani na tumbo ili kuondoa attention kifuani na kuvaa nguo za kuvuta attention chini kwa kuvaa nguo zinazomwagika kuanzia tumboni/chini ya kifua.
Nguo za shingo za V zinafaa.
Vaa sidiria zinazofit na kufanya kifua kichongoke
Kuficha hips ndogo vaa sketi au magauni yanayojaa au ya kumwagika kiunoni kwenda chini

Kundi la pear
Kundi hili vipimo vya juu ni vidogo kuliko vipimo vya chini, hivyo huwa na hipsi zenye size kubwa kuliko kifua/mabega na kiuno kidogo kuliko kifua na miguu mifupi. . kwa waafrika hii ni shape inayochukuliwa vizuri hivyo mtu anaweza akachagua aidha kulionesha umbo kama lilivyo au kubalance unene wa juu na wa chini na kuonesha wembamba wa kiuno
Ili kupunguza muonekano wa wembamba wa juu mtu wa umbo hili anaweza kuvaa nguo za juu zenye layers za material, yaani mikato yenye vitambaa kadhaa: hii inaongeza unene wa umbile la juu hivyo kubalance mwili juu na umbile la chini.

Kundi la Hour glass
Kundi hili vipimo vya kifua na hipsi vinalingana au kukaribiana sana lakini kiuno huwa kidogo yaani kilichojitenga kutokana na kuwa kidogo yani namba 8 na huwa na miguu minene.
Wengi wa kundi hili wanaweza kuvaa nguo za aina tofauti tofauti kwa kuwa miili yao inaonekana imebalance.

kundi la rectangle
Kundi hili vipimo vya kiuno na hipsi havipishani sana, vuta attention kwenye kiuno kwa kutumia mikanda ili kutengeneza curves/mgawanyiko wa maumbile.
Vaa sidiria zinazofit na kufanya kifua kichongoke
Kuongeza ukubwa wa hips vaa sketi au magauni yanayojaa kiunoni kwenda chini 

 
Top