Baraza la Mitihani Tanzania leo limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa mwaka 2016 huku ufaulu ukiwa umeongezeka kwa asilimia 2.52  ukilinganisha na ufaulu wa mwaka jana huku shule ya msingi Kwema iliyoko Mkoani Shinyanga ikiongoza Kitaifa.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania  Dr Charles Msonde amesema kuwa jumla ya watahiniwa 555,291 kati ya 7789,479 waliofanya mtihani huo wamefaulu huku huku idadi hiyo ikiwa ni sawa na asilimia 70.36 ambapo kati yao wasichana wakiwa ni 283,751 huku idadi ya wavulana ikiwa ni 271,540.

Dk. Msonde pia alizungumzia baadhi ya shule zilizobainika kufanya udanganyifu na kufutiwa matokeo yao.
Shule kumi bora zilizofanya vizuri kitaifa katika matokeo hayo ni Kwema na Rocken Hill za Shinyanga  Mugini ya Mwanza, Fountain of Joy na Tusiime za Dar es salaam na Mudio Islamic ya Kilimanjaro. Nyingine ni Atlas ya Dar es salaam, St Achileus ya Kagera, Gft Skillfull ya Dar es salaam na Carmel ya Morogoro.

Aidha Shule kumi zilizofanya vibaya katika matokeo hayo ni Mgata ya Morogoro, Kitengu Morogoro, Lumba chini Morogoro, Zege ya Tanga na Kilole pia ya Tanga. Nyingine ni Magunga ya Morogoro, Nchinila ya Manyara, Mwabalebi ya Simiyu, Ilorienito ya Arusha na Chochero ya Morogoro.

Kwa kutazama matokeo hayo kwa kubonyeza HAPA  chini..


au
 
Top