AMINI usiamini maisha yangekuwa magumu sana kwa watu wenye ubovu
wa macho kama kusingekuwa na miwani inayowawaezesha kusoma na kuona vitu
vilivyo mbali ya upeo wa kawaida wa macho yao. Kama hujaelewa bado embu fikiria
yule mtu anayepata shida kusoma katika karatasi jeupe wakati wa jua anavyoweza
kupata tabu kuona maandishi makubwa yaliyoandikwa katika karatasi hiyo. Sipati
picha jinsi watu hawa wangekuwa wanahangaika kupata taarifa mbalimbali za
kimaendeleo, kwa kweli ni shida sana kulifikiria hili.
hii ndio list ya misimu ya miaka inavyofuatana katika maendeleo |
Stori inatupeleka katika miaka ya 1000 kabla hata ya wakati wa
kawaida,ambapo kionea mbali cha kwanza kilivumbuliwa.
Katika mwaka wa 1284 muitaliano Salvino D’Armate alikuja
kutengeneza miwani ya kwanza ya kuvaa na ndipo ukombozi wa watu wenye ubovu wa
macho ulipoanzia hapa.
Karne nyingi hata mara baada ya wakati wa kawaida kuanza
kuhesabiwa,miwani imekuwa msaada mkubwa kwa watu mablimbvali iwe watoto au
wakubwa.
Karne ya 13 inaelezwa kuwa ndiyo ilianza kuubadili kidogo
muonekano wa miwani kwani lensi yake ilikuwa na mabadiliko kidogo tofauti na
lensi ya awali
Katika kipindi hiko pia miwani ilianza kutumika pia katika
kusomea maandishi mbalimbamli na picha ambazo zilikuwa zikiandikwa katika safu
za milima.
MIWANI YA JUA
Mwaka 1752,Bwana James Ayscough alikuja na ubunifu wa kuyafanya
miwani imrahisishie si tu mtu mwenye tataizo bali watu wote ambao hutatizwa na
miali mikali ya juaInaelezwa kuwa miwani ya jamaa huyu ilikuwa ikifanana kwa
kiasi kidogo na miwani ya wakati huu,
Mwaka 1919 kampuni kubwa ya kutengeneza,kuuza na kusambaza
miwani ya Foster Grants ilizinduliwa,kampuni hiyo ilikuwa na kazi ya kuuza na
kusambaza miwani hiyo ya jua katika sehemu kubwa ya bara la Ulaya na Marekani.
Leo
hii ulimwengu unashuhudia mabadiliko makubwa ya miwani ambapo kuna hadi miwani
ambayo inakamera ambayo inamwezesha mtu kurekodi video wakati anatembea.
Aidha
baadhi ya miwani pia inampa mtu uwezo wa kultazama jua moja kwa moja bila hata
kuathirika na mionzi mikali ya jua.