Nyanya chungu au ngogwe ni tunda ambalo wengi
tumekuwa tukilitumia kama mboga au kiungo kimoja wapo katika kunogesha mboga
lakini wachache mno wanaojua faida zake kiafya.
Pamoja na kufanya mboga kuwa na ladha na harufu ya
aina yake, nyanya chungu zina kazi kubwa katika mwili wa binadamu ikiwa ni
pamoja na kujenga na kuimarisha afya ya mlaji.
Nyanya
chungu ipo kwenye kundi la mbogamboga zenye virutubisho vingi vikiwemo vitamin
A, B, na C ambazo zote kwa pamoja hufanya kazi ya kuboresha afya ya mwili kwa
ujumla.
Ndani ya
nyanya chungu pia kuna Vitamin K inayosaidia kuipa nguvu mishipa ya damu hivyo
kusaidia zoezi zima la mzunguko wa damu katika mwili wa binadamu.
Licha ya
kuwa karibu asilimia 90 ya nyanya chugu ni maji, mboga hii ina madini ya chuma
na potassium hivyo kusaidia uimara wa mifupa.
Nyanya
chungu pia husaidia kuimarisha kinga ya mwilli na kumsaidia mlaji kuepukana na
magonjwa ya mara kwa mara.
Mboga hii
pia ni kinga inayoweza kumuepusha mlaji kupata maradhi ya moyo au tumbo kujaa
gesi au hutoa kinga kwa wanaume wasipate na ugonjwa wa ngiri.
Kwa
wagonjwa wa kisukari, nyanya chungu ni dawa inayoweza kusaidia katika kupunguza
kiwango cha sukari mwilini,
Katika uzazi na nguvu za
kiume
Ngogwe au nyanya chungu husaidia sana katika
kuongeza nguvu za uzazi kwa wanaume na inatibu pia wale wenye ugonjwa wa ngiri. Mbali na sifa hiyo ya ngogwe / nyanya chungu pia husaidia kuongeza stamina na uwezo wa kuvumilia na kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu kati ya mume na mke wote endapo watakuwa wanatumia nyanya chungu katika utaratibu unaotakiwa kitaalam (mchemsho) .
hivyo basi katika chakula chako ni muhimu sana kula
nyanya chungu japo kwa wiki mara mbili au tatu kutokana na faida zake kama
tulivyoainisha hapa
jiunge nasi
fb@edonetz twiter@edonetz inst@edonetz_blog na youtube@edone tv