Chunusi ni ugonjwa
wa ngozi ambao hujitokeza kama viuvimbe au vipele vidogo vidogo hasa sehemu za
uso, kifuani na hata mgongoni.
Vipele hivi hutokea wakati vishimo vya
kupitisha jasho katika
ngozi vinapozibwa kwa mafuta au seli za ngozi zilizokufa au wadudu yaani
bakteria.
Kwa lugha ya
kidaktari chunusi huitwa Acne
Vulgaris. Chunusi ndio
ugonjwa wa ngozi ambao humwathiri binadamu kwa kiasi kikubwa kwa mfano nchini
Marekani pekee huathiri watu zaidi ya milioni 17.
Chunusi huweza
kujitokeza katika umri wowote lakini huathiri sana vijana hasa wakati wa balehe
(adolescents).
maji ndio kitu mhimu
kabla ya kwenda nbali
tuanze na hili jambo la muhumu kwa mtu anayesumbuliwa na chunusi ni kunywa
maji kwa angalau lita 3 kila siku pia ni muhimu sana kwa ngozi yako, matunda
fresh na mboga za majani kwenye diet yako.
1. Magadi Soda:
Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso
na haswa ukiwa na chunusi.
Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo
na kisha weka au kandika kidonge hicho sehemu iliyoathirika na chunusi.
Kwa muda wa dakika 15 hadi
20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa majiyasiyo ya moto. Unaweza kurudia rudia
mara kadhaa kwa siku mpaka utakapoona athari za chunusi zimepotea.
2. Matango:
Unaweza kutumia Tango kwa
kuondoa chunusi na
hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana
yenye afya na yenye
kuvutia.
Matango ni mazuri sana kwa
kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na
kisha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Acha
likae kwa muda wa dakika 15 hadi 20 hivi, kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku
mara mbili mpaka mara tatu hadi utakapopona.
3. Kitunguu Swaumu:
Unaweza kutumia kitunguu
swaumu kuondoa chunusi.
Matumizi ya Kitunguu swaumu huleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusiusoni na hata
kuuwa bakteria sababu kina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria
kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata
kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili ya
kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili).
Twanga kitungu swaumu, au
unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi huku
ukishikilia kwa dakika 5 mpaka 10, na kisha safisha namaji baridi. Waweza kufanya hivyo
asubuhi na jioni.
4. Mnanaa (Peppermint):
Unaweza kutumia majani ya
Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya mnanaa hutumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa.
Twanga majani machache au
saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha
kwa maji baridi. Unaweza
kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.
5. Limao:
Kata limao na kisha kwa
kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwenye majiya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha acha
pakauke, unaweza kurudia rudia kila baada ya masaa kadhaa.
Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa (ya
dukani), kwa sababu yanaweza kuwa yamewekwa kemikali zingine ili kuyahifadhi
kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao halisi.
6. Asali:
Matumizi ya asali kutibu chunusi huwezesha
ngozi, iwe na afya na
nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna
virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na
kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na
iache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata
mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na
kuifanya iwe na afya na
mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza
kusafisha kwa kutumia maji ya
vuguvugu.
7. Papai:
Unaweza kushangaa, lakini
matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na
kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha
papai na upakae sehemu yenye chunusi, kisha liache
kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kujisafisha kwa
kutumia maji ya kawaida.
Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.
8. Dawa Ya Meno:
Unaweza kushangaa, lakini
ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa
Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine.
Tumia dawa ya meno
isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri
ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa
asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze
kufanya kazi vizuri.
Namna nyingine ni
kuchanganya dawa ya meno
na unga wa mahindi au ngano iliyosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na
kuiacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.
9. Poda:
Unaweza kutumia baby
powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na kuiacha
mpaka asubuhi.
10. Mvuke:
Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi
kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine
wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo
huku ukielekeza uso wako kwenye sufuria au bakuli lenye majiyanayotoa mvuke kwa dakika 5 mpaka 10
hivi. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.
ZINGATIA:
Kunywa maji ya kunywa kila
siku glasi 8 mpaka 10, jishughulishe namazoezi ya viungo na
ujiweke msafi kila mara.
Njia hizi za Asili zinaweza
kuchukuwa muda kidogo mpaka kuona matokeo ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama
hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali
iliyo karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.