Ngozi
nyeusi katika magoti na nyuma ya mikono hutokana na mkusanyiko wa cells
zilizokufa, na hata unavyoweka pressure kwenye magoti na vipepsi vya mikono
yako. Kama ukiwa unaweka mikono kwenye meza
ukiwa kazini, ule msuguano unafanya
ngozi iwe nyeusi.
Kama una
magoti myeusi na nyuma ya mikono pia ni peiusi, tumia hizi njia asili kuweza
kuondoa weusi huo::
Tumia Aloe Vera Juice
Juice ya
Aloe Vera inasaidia kuondoa weusi, cha kufanya ni kupaka juice hiyo
kwenye sehemu yenye weusi na uache kwa nusu saa kisha nawa na upake
moisturizer. Rudia kufanya hivi mara mbili kila siku.
Tumia Binzari Manjano, Asali na Maziwa.
Changanya
vyote hivi utapata mchanganiko mzito, paka kwenye magoti na kwenye mikono yako
palipo na weusi. Kaa nayo kwa dakika 30, nawa na paka moisturizer. Rudia hii
kila siku kwa wiki 3-4, utapata matokeo mazuri.
Tumia Ndimu.
Chukua
pamba na uitumie kupaka juice ya ndimu katika sehemu zenye weusi. Au unaweza
kuikata tu ndimu na kuipaka directly kwenye sehemu zenye weusi. Kaa nayo kwa
lisaa 1 kisha nawa. Rudia hivi kila siku hadi weusi utakapopotea.
Tumia Olive Oil na Sukari.
Changanya vizuri, hii itakuwa
kama exfoliation/scrub kwa ajili ya magoti na mikono. Paka katika hizo sehemu
zenye weusi kisha kuwa kama una-massage polepole. nawa kwa maji ya uvuguvugu
kisha paka moisturizer.
jiunge nami katika facebook na tweter natumia @edonetz ,instergram edrickdawson
www.edonetz.blogspot.com