Tumezoea ikifika jioni utasikia mzazi akiwaambia watoto wake oga mapema ukalale mapema swali ni je? muda mzuri wa kulala ni saa ngapi? soma hapa leo.... 
Wanasayansi wa idara ya utafiti kuhusu usingizi nchini Marekani wamefanya utafiti kuhusu muda wa kulala unaofaa kwa watoto wenye umri tofauti.
Utafiti huo umebaini muda wa kulala unapungua hatua kwa hatua kufuatia kuongezeka kwa umri wa watoto. Watoto wachanga wenye umri wa miezi minne hadi mwaka mmoja wanatakiwa kulala saa 12 hadi 16 kwa siku, wale wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi miwili wanatakiwa kulala saa 11 hadi 14, umri kati ya miaka mitatu hadi mitano wanatakiwa kulala saa 10 hadi 13, na umri kati ya miaka 6 hadi 12 wanatakiwa kulala saa 9 hadi 12. Watoto wanahitaji muda wa kulala usiopungua saa 8.

Pia utafiti unaeleza wakati binadamu wanapolala, hali ya miili na akili inafufuka. Kutolala kwa muda wa kutosha kunaongeza hatari ya kupata magonjwa mbalimbali, yakiwemo kunenepa kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari na mfadhaiko.
jiunge nasi 
fb@edonetz, twiter@edonetz,inst@edonetz_blog na youtube@edone tv
 
Top