Ukiongelea mapenzi unaongelea kitu kikubwa sana kinachoteka akili na hisia za kila mmoja hapa dunia na hakuna jinsi ya kuya kwepa mapenzi,kutokana na watu wengi kushindwa kuwamudu wapenzi wao na wengine kuishia kulalama tu bila kujua tatizo wala mwarobaini wa kutatatua tatizo hili,sasa leo naomba muda wako tujadili haya ukiyafuatilia vizuri itakusaidia ukishamuonyesha kuwa unamfanyia yafuatayo kama 

1. UNAMJALI

Hakuna kitu kizuri kama kujaliwa na unayempenda na ndio kitu muhimu sana kwenye mapenzi. Ukionyesha kujali kwenye mapenzi basi hata vitu vingine vingi huenda kwenye mstari ulio salama na hufanya mapenzi yenu kuwa nyoofu siku hadi siku.

2. UNAMSAIDIA

Hiki pia ni kitu bora sana kwenye mapenzi hasa kwa kutambua kuwa mojawapo ya njia nzuri za kudumisha mapenzi ni pamoja na kusaidiana pale linapotokea tatizo lolote lile kwa mmojawapo kati yenu. Jitolee kwa kila khali kwa mpenzi wako pale anapopata shida/tatizo lolote.

3. UNAMRIDHISHA

Ni kitu safi sana kuwepo kwenye mahusiano ambayo kila mtu anaridhika na mwenzake. Iwe ni kwenye mambo ya kawaida au hata yale mambo ya ndani. Ukiridhika na huyo uliyenaye na ukaridhika kwa kila anachokupa basi mapenzi huenda murua kabisa.

4. UNAMTETEA

Unapoonyesha kuwa upande wa mwenzi wako kwenye kila tatizo au challenge yoyote inayotokea basi huwa ni njia nzuri sana nay a msingi kudumisha mapenzi yenu. Kuna mengi yanatokea kila siku kwenu ila jitahidi kila mara kumtetea kwa lolote mbele yake isipokuwa tu labda liwe kweli amekosea na hapo mrekebishe katika hali ya kimapenzi zaidi bila kumkwaza.

5. MVUMILIVU/HUNA TAMAA

Hii ni kitu njema sana nay a busara sana kwenye mapenzi na hupendwa hasa na sie wanaume pale linapokuja suala la mahusiano ambapo huwa tunapenda sana wanawake wasio na tamaa na ni wavumilivu kwa lolote ndani ya mapenzi. Hatupendi wasichana wanaoshoboka kwa vitu vidogo na vya muda na kuishia kuharibu mapenzi.

6. UNAMPA CHANGAMOTO

Unapokuwa kwenye mahusiano haina maana basi kila anachofanya mpenzi wako ni sahihi hata kama unaona anakosea. Kama unaona hayupo kwenye njia sahihi basi mpe ushauri/changamoto ili aweze kubadilika na sio kila kitu kuwa mtu wa kumuitikia ‘’NDIO’’ tu kitu ambacho hakijengi bali kinabomoa

ungana nasi
fb@edonetz,twiter@edonetz, inst@edonetz_blog na youtube@edone tv


 
Top