nitakuwa nakukusanyia story zote kubwa za burudani na kukuwekea hapa kila siku tuanze na hii....


Babutale  eti Kama ni rahisi kununua tuzo, wanaosema hivyo na wao wakanunue  
Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.
Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.
Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.
Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.
Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.
P-Funk tayari ameshampata msichana wa kwanza kumsainisha Bongo Records
Kwa muda mrefu, producer mkongwe wa Bongo Flava, P-Funk Majani alikuwa akizungumza nia yake ya kupata wasanii wa kike kwaajili ya kuwasainisha Bongo Records.
Na sasa ametangaza kumpata msichana wa kwanza atakayemwagika wino kuwa chini ya usimamizi wa label yake kongwe. Anaamini kuwa msichana huyo atafanya mambo makubwa.
“I finally found the perfect female artist to sign to Bongo Records. She’s gonna take over the music industry by storm,” ameandika Majani kwenye picha ya msichana huyo aliyoiweka Instagram.
“What do you think, does she rap or sing,” amehoji.
Hivi karibuni Majani alisema anatarajia kutambulisha vipaji vipya takriban vinane vitakavyokuwa chini ya label yake.
Mpango huo aliutambulisha takriban miaka miwili iliyopita na kupata wasanii lakini alikosa muda wa kuendelea baada ya kupata majukumu ya kampuni ya CMEA.
Na sasa amesema ameshakutana na wasanii hao tena na kuongeza wengine tayari kwa kuufufua mradi huo.
“Tuseme wako kama nane kwahiyo sasa hivi ndio tupo studio tunajifua, kila mmoja anapiga kazi tatu tatu then tutawaalika watu wa media, watu wa industry, tutakaaa tutakagua zile nyimbo na nyinyi mtapata nafasi sasa ya kuchagua single zao ambazo sasa tutainvest, tutaingia kwenye videos na tutazazimarket zile.”
Alidai kuwa bado anaendelea kusaka vipaji zaidi na kwamba angependa kupata wasanii wa kike zaidi.
EFM wamkwapua Twalib Omar wa Clouds TV
Vita vya EFM NA Clouds Media vinazidi kushika kasi. Baada ya Clouds FM kumrudisha mtangazaji wake wa zamani, Paul James aka PJ wiki kadhaa zilizopita, EFM wamejibu mapigo kwa kumchukua mtangazaji wa Sports Bar ya Clouds TV, Twalib Omar.
Twalib hajamaliza hata miezi minne kama sio mitatu Clouds TV alikoenda baada ya kuondoka Azam TV.
Usajili huo mpya umetangazwa na Maulid Kitenge ambaye kupitia ujumbe wake wa Instagram, inaonesha amempiga kijembe hasimu wake, Shaffi Dauda ambaye ni meneja wa vipindi wa Clouds FM.
“Wakati unahangaika kurudisha wale wa zamani siye tunakuchukulia wengine,” ameandika Kitenge.
“Karibu jembe Twalib Omar E FM na hii jezi utaitumia katika E FM jogging club yetu. #huumchezohauitajihasira msalimieni rafiki yangu Mino Raiola mwambieni kuna Jorge Mendez yeye harudishi wa zamani anachukua wapya,” ameongeza.
Hadi sasa watangazaji wengine wa Clouds FM waliopo EFM ni pamoja na Dina Marious, Gerald Hando na Ibrahim ‘Maestro’ Masoud. Pamoja na kuwarudisha watangazaji wake wa zamani Gardiner G Habash na PJ, Clouds ilimkwapua mtangazaji wa Singeli, Kicheko kutoka EFM.
Views ya Drake yaweka rekodi mpya kwenye mtandao wa Spotify
 
Kuizuia nyota ya Drake ni sawa na kuziba mwanga kwa kiganja cha mkono. Album yake ya Views, imekuwa ya kwanza katika historia kusikilizwa mara milioni 880 kwenye mtandao wa Spotify.
Rapper huyo wa Canada ameweka rekodi hiyo ikiwa ni wiki chache zimepita tangu mtandao wa Apple Music ulipotangaza albamu hiyo kuweka historia ya kusikilizwa mara bilioni 1 kwenye mtandao huo.
Drake ameweka rekodi hiyo kwenye mtandao huo wa Spotify baada ya kuivunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa mwaka uliopita na Major Lazer, DJ Snake na MØ’s na wimbo wa ‘Lean On’ iliyosikilizwa mara milioni 526.
Lulu awataja wasanii 3 anaowakubali kwenye Bongo Fleva
Msanii mahiri wa filamu Bongo, Elizabeth Michael aka Lulu amewataja wasanii watatu anaowakubali kwenye muziki wa Bongo Fleva.
 
Muigizaji huyo alikuwa akijibu swali la mmoja wa mashabiki wake kwenye mtandao wa Twitter, lililokuwa linauliza “wasanii gani watatu anaowakubali kwenye Bongo Fleva?”
Lulu alijibu swali hilo kwa kuandika, “Beka, Maua Sama na Alikiba.”
 
Lulu aliongeza kwa kuzitaja nyimbo anazozikubali ni pamoja na ‘Ado Ado’ wa Mo Music, ‘Wale Wale’ wa Ruby, ‘Hapo’ wa Quick Rocka na ‘Asanteni Kwa Kuja’ wa Mwana FA.
 Yaliyosemwa na Vanessa Mdee jinsi alivyoandika wimbo mpya wa Mafikizolo..
 
Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni kundi la muziki kutoka Afrika Kusini, Mafikizolo lilitangaza kuachia wimbo wao mpya walioupa kwa jina la ‘Kucheza’.Sasa basi good news ni kwamba Vanessa Mdee amehusika katika single hiyo kama mtunzi huku ikiwa imetayarishwa na Dj Maphorisa wa South Africa.

Vanessa Mdee ameongea yafuatayo “Ilikuwa ndoto yangu kufanya kazi na Mafikizolo  sikutegemea kabisa kuandika wimbo wa Mafikizolo ambao watautoa kama wimbo wao mpya uitwao Kucheza, pili ningependa kumshukuru Dj Maphorisa kwani alinipa mawazo tofauti tofauti kipindi tulipokuwa studio baadae Mafikizolo wakaukubali kwahiyo nitahusika kama mtunzi kwenye wimbo wao mpya’”
 
Top