Tumezowe kuona mama mjamzito akila sana udongo japo pia wapo ambao hua wanakula licha ya kuwa si wajawazito. Yawezekana hawa woote wanakula kutokana na hamu ambayo husikia pasipo kujua kuwa madhara yake ni makubwa kushinda hiyo hamu ambayo uwezo wa kuijuia upo chini ya mtumiaji.

Tuanze na Utafiti  unasemaje ……
Wanawake wanaokula udongo wakiwa wajiwazito wamo katika hatari ya kuwafanya watoto watakowajifungua kutofanya vizuri shuleni.
Utafiti uliofanywa na shirika la African Council for Gifted and Talented unaonyesha kuwa watoto ambao kina mama wao walikuwa wakitumia udongo hawamakiniki darasani.
Mkuu wa shirika hilo Profesa Humprey Obora amewaambia wanahabari jijini Nairobi kuwa utafiti huo umefanywa kwa watoto wanaopelekwa katika taasisi hiyo ambayo hujihusisha kutambua na kukuza vipawa vya watoto wakiwa bado wachanga.
Kwa kawaida wanawake wengi hutumia udongo huo baadhi wakidai kuwa wana upungufu wa madini ila wengi wao huzidisha matumizi yake.
Zaidi ya wazazi 4000 walihusishwa katika utafiti huo lakini ni 1000 tu ambao maoni yao yalitumika kuandaa ripoti ya utafiti huo.
Taasisi hiyo ilikuwa ikifuatilia matokeo ya watoto hao wakiwa shuleni kwa muda wa miaka minne na wakatambua kuwa wale ambao hawakuwa imara darasani mama zao walikuwa na historia ya kutumia udongo wakiwa wamebeba mimba zao.
Watafiti hao wanasema kuwa kutokana na hayo ubongo wa watoto waliozaliwa hao huchelewa kushika mambo.
Wasimamizi wa mradi huo waliwahusisha wazazi kutoka katika sehemu mbalimbali nchini Kenya ambako kuna vituo vya shirika la African Council for Gifted and Talented.
Kadhalika utafiti huo unaonyesha kuwa wanawake katika miaka ya ishirini huwa na hamu kubwa kutumia udongo.

Hili ni tatizo la kupenda kula vitu ambavyo si chakula kama vile udongo, mshumaa, mkaa, chaki, karatasi, kucha, majivu na vitu vingine. Mtu yeyote anapotamani kula au kula vitu hivi kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja endapo umri wake ni zaidi ya miezi 24 kwa maana ya miaka miwili ni wazi kuwa ana tatizo la ugonjwa ujulikanao kitabibu kama ‘PICA’.
Ugonjwa huu huwapata sana wanawake na wasichana hasa pale wanapokuwa wajawazito. Kula udongo na vitu vingine ambavyo si chakula kunaweza kusababisha madhara ya kiafya kutokana na ukweli kuwa udongo unaweza kuwa na sumu za dawa za mimea na mbolea. Sumu kama lead, dioxin na madini mengine yenye hatari yanayopatikana kwenye udongo uliochafuliwa, husababisha matatizo ya kiafya.
……………………..
kusababisha mikwaruzo, michubuko na kupata majeraha ya ndani kwenye utumbo.
Ugonjwa wenye homa na maumivu makali unaojulikana kama appendicitis ambao tiba yake ni upasuaji.
Na pia udongo una uchafu wa kila aina vikiwemo vijidudu vya bakteria na mayai ya minyoo, hivyo kuutumia kama chakula ni hatari kwa afya ya wewe utumiaye.

Tabia hii ya kula vitu ambavyo si chakula imekuwa ni chanzo cha magonjwa kama vile saratani ya tumbo, minyoo na madhara ya kiafya yatokanayo na kuharibika kwa ini. Watu wanaokula vitu hivi hukabiliwa na tatizo la kujaa kwa tumbo na kuvimba, kutopata choo na tumbo kuuma kwa siku nyingi bila sababu bayana. Mara nyingi udongo huchafuliwa kwa vinyesi na mikojo ya binadamu, ndege na wanyama kama mbwa nk, hii husababisha udongo kubeba vimelea vya magonjwa.
Wasichana wengi wanaokula vitu ambavyo si chakula hukabiliwa na tatizo la upungufu wa madini chuma na zinc mwilini. Hii ni kutokana na lishe duni au kupoteza damu nyingi wakati wa hedhi au upungufu wa madini chuma kutokana ugonjwa wa minyoo ya safura. Ulaji mbaya kama vile kunywa chai yenye majani ya chai au kahawa wakati wa kula huzuia madini ya chuma kufyonzwa au kusharabiwa na kuingia mwilini. Upungufu wa dawa ya kuyeyusha chakula tumboni (hydrochloric acid) pia husababisha tatizo hili.
Tatizo la kula vitu ambavyo si chakula pia huusishwa na magonjwa ya akili hasa kwa watoto wadogo. Kwa akina mama watu wazima tatizo hili pia linaweza kusababishwa na kutokwa jasho jingi kila siku. Jasho jingi hupoteza takribani gram 15 za madini chuma mwilini kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Vyanzo vingine vya upoteaji wa madini chuma mwilini ni kupotea kwa damu muda mrefu na kidogo kidogo wakati wa hedhi isiyo na mpangilio, saratani ya mji wa kizazi, malaria sugu, kichocho, bawasili (haemorrhoid), kuharisha damu na vidonda vya tumbo.
 Mimba za mara kwa mara na kunyonyesha pia hupoteza madini ya chuma mwilini.
Inakadiliwa kuwa mwanamke anayejifungua inamchukua miaka miwili kurejesha gram moja ya madini chuma yaliyopotea toka mwilini wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Hali hii inaweza kuwa mbaya zaidi kwa wasichana wanaopata mimba katika umri mdogo.
Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili kukabiliana na tatizo hilo:
• Kula vyakula vyenye madini chuma na zinc kwa wingi kama vile maharage, korosho, mboga za majani hasa spinach, mayai, nyama, samaki, mbegu za maboga na matunda.
• Kutibu minyoo kwa kumeza dawa za minyoo angalau mara moja kwa mwezi.
• Kunywa juice ya spinach na karoti bilauli moja kutwa mara tatu kila siku. Kunywa supu ya mbogamboga na mchele.
• Usinywe vinywaji vyenye caffeine wakati wa kula chakula.
• Meza dawa zinazoongeza madini chuma mwilini kama vile ferrous sulfate nk.
• Safisha misumali kwa maji moto, iloweke kwenye maji ya limao kisha tengeneza juice kwa maji haya na unywe mara kwa mara au pika chakula kwa kutumia sufuria ya chuma.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW

FACEBOOK@EDONETZ  ,TWITER@EDONETZ INSTAGRAM@EDONETZ NA YOUTUBE@EDONETZ TV
 
Top