Kitu cha
kwanza lazima tujue kwamba Kwikwi ni ugonjwa. Pengine labda hujawahi kutilia
maanani hali hii ambayo hukufika mara chache sana. Lakini ukweli ni kwamba kuna
watu wanaathirika na kwikwi kwa kiasi kikubwa zaidi ya wengine.
jinsi kwikwi inavyotokea |
Hebu tuanze
kwa kuangalia story hii.
Bwana
mmoja aitwaye Charles Osborne kutoka katika jimbo la Iowa, Marekani, alianza
kutoa mlio kwa kwikwi (hiccupping) mnamo mwaka 1922 na kuendelea hivyo kwa muda
wa miaka 65. Mpaka kufariki kwake, Bw. Osborne alikuwa amepiga kwikwi takribani
milioni 430! Ndio ujue sasa na ujiulize wewe ushapiga kwikwi mara ngapi.
Kwanza inbidi tujue kwamba Kwikwi
ni tendo lisilo la hiari la kusinyaa kwa kiwambo cha mapafu (diaphragm) likifuatiwa na kufunga kwa
haraka kwa koromeo linalopitisha hewa.
Nini
husababisha Kwikwi
Sababu
kuu mbili zinazopelekea kupatwa na kwikwi ni kula na kunywa kwa
kupitiliza. Ulaji wa chakula au unywaji wa vimiminika kwa kiasi kikubwa
husababisha tumbo kutanuka kuelekea chini na kujikandamiza dhidi ya kiwambo
(diaphragm) ambako hupelekea kuanzishwa kwa mtetemo wa kwikwi.
Sababu
nyingine zinazpolekea wewe kupatwa na kwikwi ni:
Kula
chakula kwa kasi kubwa
Kuhamaki
kwa hasira pasipo na sababu kubwa
Kula
chakula kusikofuata ratiba maalum
Kunywa
vinywaji vya chupa kama vile soda
Msongo
wa mawazo au mshawasha juu ya jambo fulani
Kuoga
maji ya baridi sana
Kuvuta
sigara
Kunywa
pombe kali
Kunyonyesha
mtoto kwa mama mzazi kwa sababu mtoto anaponyonya anavuta hewa
Njia za
Asili za kukabiliana na Kwikwi
Njia
zifuatazo zitakusaidia kukabiliana na kwikwi. Njia hizi zinahusisha kuifanya
kwikwi kutulia kwa kufanikiwa kupindisha njia ambayo inapelekea kwikwi kutokea.
·
Chukua bahasha kubwa (A6). Hizi zinapatikana maduka ya vifaa vya
ofisini, rangi ya khaki. Uweke mdomo wako katika bahasha, hakikisha unaziba
vizuri pasiwe na namna hewa inaweza kuingia ndani ya bahasha.
·
Pumua ndani ya bahasha, kwa kuvuta na kutoa hewa mara 10, mpaka
uhisi kuishiwa pumzi. Unapopumua ndani ya bahasha, unatengeneza hewa ya ukaa
ambayo inajulikana kama kikwazo cha kwikwi.
·
Vuta hewa na ishikilie katika mapafu kwa kadiri unavyoweza kisha
imeze unapohisi kwikwi inataka kurejea tena. Fanya hivi mara 2 mpaka 3. Baada
ya hapo tulia na rudia tena.
·
Vuta na shikilia hewa katika mapafu yako kwa muda mrefu kadiri
unavyoweza kisha iachie kwa kupumua taratibu.
·
Pumua taratibu, ukiwa umekaa wima kadiri uwezavyo
·
Ishikilie hewa katika mapafu yako huku ukiinamisha kichwa kwa
nyuma mpaka umbali unaoweza.
·
Meza kijiko kimoja cha sukari nyeupe. Hii husaidia kusimamisha
kwikwi ndani ya dakika chache.
·
Ziba mdomo wako, nyanyua mikono yako na ziba matundu ya pua kwa
vidole vya mwisho huku wakati huo huo ukiziba masikio yako kwa vidole gumba
kisha vuta hewa mara 3 kabla ya kuachia. Hii hutengeneza ombwe dogo ndani ya
mapafu na kusababisha mabadiliko katika mzunguko wa kiwambo.
·
Tafuna barafu taratibu na imeze kwa dakika 10 mpaka 15.
·
Simama nyuma ya mtu mwenye kwikwi, akiwa ameketi katika kiti.
Ishike shingo yake taratibu kwa kutumia vidole vyako kisha mkande kande upande
wa nyuma wa shingo yake, kila upande wa uti wa mgongo, kwa kutumia vidole
gumba.
·
Jaza maji ya kunywa katika glasi, inama kuelekea mbele kisha
kunywa maji hayo kinyume.
·
Chukua kiganja cha mkono wako na kigandamize katikakati ya kifua
chako, kwenye mfupa ulio karibu kabisa na tumbo lako.
·
Weka barafu kwenye shingo yako
·
Kunywa maji mafundo 10 mfululizo bila kupumua
·
Kunywa maji huku ukiwa umeweka mdomoni mwako kalamu ya mkaa
iliyoshikiliwa na gego la mwisho.
·
Lala ubavu wako wa kushoto kwa dakika 10 mpaka 15.
·
Piga kelele au imba kwa sauti ya juu kadiri unavyoweza
·
Mwambie rafiki au ndugu yako akukande kande miguu
·
Kunywa nusu glasi ya juisi ya machungwa
·
Oga maji moto kwa dakika 15
·
Loweka miguu yako kwenye beseni la maji kwa dakika 15.
·
Jiinamishe na gusa vidole vya miguu kwa vidole vyako vya mikono,
kaa katika pozi hili kwa sekunde 60. Njia hii ni nzuri kwa watoto na watu
wazima.
·
Watoto wanapocheza na kukimbizana, mara nyingi hujikuta
wakipatwa na kwikwi. Jambo hilo likitokea, jaribu kumtekenya mwanao huku akiwa
ameshikilia hewa (yaani asipumue). Hakikisha unamsisitiza asicheke. Atasahau
kabisa juu ya kwikwi.
·
Unapokula chakula, jaribu kuwa kimya, uwezekano wa kupatwa na
kwikwi ni mdogo.
·
Kama una kwikwi zinazodumu, funga kwa siku tatu mfululizo,
ukinywa juisi za matunda pekee.