kwanza tambua kuwa jinsi wanaume wanavyobeba vyuma na kuongeza vifua na mikono
hivyohivyo wanawake wanaweza kuongeza misuli hiyo muhimu ya makalio ambayo
kitaalamu inaitwa gluteal maximus,gluteal minimus na gluteal medias. hiyo ndio
misuli mikuu mitatu ambayo kwa pamoja inaitwa makalio na ikifanyiwa mazoezi
vizuri huongezeka na kua mikubwa.
Ni kweli ukubwa wa makalio na kiungo chochote cha mwili hufuata
ukoo lakini pia mazoezi husaidia sana kukuza makalio au kiungo chochote cha
mwili chenye misuli sio kua makubwa tu hata kuyafanya kua na shepu nzuri na
kuvutia..
Unaweza kua hujaamini bado lakini kwa kukuthibitishia habari
hizi ni kwamba jeniffer lopez mwanamuziki na muigizaji wa filamu nchini
marekani ambaye anaongoza kwa kua na makalio makubwa zaidi kuliko wasanii wote
mpaka akayakatia bima yaani insurance anafanya mazoezi haya kama ifuatavyo..nakusihi
fuata maelekezo yafuatayo..
Mazoezi ya squat; mazoezi haya huanzwa kwa
kusimama na miguu yote miwili kisha kuanza kama unakaa hewani halafu unainuka,
mazoezi haya huvuta misuli ya makalio na kuibana kisha kuongeza upana na siku
za kwanza za mazoezi haya mtu hujisikia maumivu na kuanza kuhisi nguo zimeanza
kubana mpaka mapajani. ni zoezi kuu na muhimu katika kukuza makalio.fanya zoezi
hili kwa raundi tatu kila raundi fanya mara kumi na tano au unaweza ukaanza
kama picha inavyoonyesha hapo kwa mwezi mmoja kisha ukaendelea na mazoezi ya
kawaida kama nilivyoelekeza.
donkey kick; piga magoti kisha weka mikono
chini kama mbuzi anavyosimama kisha inua mguu mmoja wa nyuma mpaka uangalie juu
kisha rudisha chini taratibu.fanya hivi raundi tatu huku kila mguu ukiinua na
kuurudisha mara 20.
zoezi
la bridge; watu wengi wanashinda wamekaa
kwenye viti mashuleni au maofisini muda mwingi na hali hii hufanya hata
mtu mwenye makalio makubwa ya kuzaliwa nayo kuanza kupoteza shepu yake nzuri ya
mwanzoni. zoezi hili huanza kwa kulala chini kwa mgongo kisha inua kiuno kwa
juu, sasa bakia kwa hali hii kwa muda kisha nyoosha mguu mmoja kwa mbele kwa
sekunde kadhaa afu rudisha chini halafu badilisha mguu.fanya hivi kwa kila mguu
mara kumi kwa raundi tatu huku ukipumzika dakika mbili kila baada ya raundi.
kula protini nyingi: vyakula vya protini ni
muhimu kujenga misuli na mifupa hivo kula sana maharage, nyama, samaki,maziwa,
karanga, korosho na kadhalika. hii itakujenga haraka sana na kukupa matokeo
mazuri kwani mwili unajengwa na chakula.
chagua aina nzuri ya wanga; ulaji wa
mikaango kama chips, chapati, maandazi na kadhalika sio wanga nzuri kwani huleta
vitambi na kukufanya ue na shepu mbaya ni vizuri kula wanga asili kama
ugali,viazi,mihogo,wali na kadhalika.
tumia mboga za majani; mboga za
majani ni muhimu sana kwani husaidia chakula ulichokula kiweze kunyonywa na
mwili kirahisi na kupunguza uwezekanao wa kupata kitambi.
tumia virutubisho vya kutosha; virutubisho
vyenye madini mbalimbali na protini ni muhimu sana kwani vyenyewe vinaenda moja
kwa moja kufanya kazi kwenye mwili na kuanza kujenga misuli hii bila kuanza
kufyonzwa taratibu tumboni kama vyakula vingine. utafiti unaonyesha wanaotumia
virutubsho hivi hufanikiwa sana kuliko wasiotumia kabisa.jinsi ya kutumia;
chota kijiko kimoja kilichowekwa kwenye virutubisho vyako kisha changanya na
maziwa kwa upande wa protein shake na kwa upande wa argi changanya kijiko
kimoja cha unga na maziwa ya mgando au juice.kunywa mara moja au mbili kwa siku
huku ukiendelea na mazoezi.
mwisho: kama ilivyokua kwa mazoezi mengine yeyote itakuchukua muda
angalau wiki mbili au mwezi mmoja kuanza kuona matokeo na haimaanishi kwamba
ndio matokeo mazuri yakipatikana ndio unaacha hapana, mazoezi ni muhimu kwa
mwili wa binadamu, unaweza ukaanza na zoezi la mwezi yaani mara moja kwa siku
kisha endelea na zoezi hili mara tano kwa wiki baada ya mwezi wa kwanza.
kumbuka kama ilivyo kwa mazoezi mengine ya mwili, unahitaji moyo wa mazoezi
kufanikiwa, usije ukafanya zoezi siku mbili ukaacha afu ukategemea
mabadiliko..unaweza ukatutafuta kupata virutubisho hivyo, kupata video za
mazoezi na kwa msaada wa kitaalamu zaidi.ahsante sana mtu mkubwa endelea kuwa nami naomba unisambazie link hii www.edonetz.blogspot.com