Banana Zorro awataja wasanii wa Bongo
Flava anaowakubali kwa kuimba live
Ukiambiwa utaje orodha ya wasanii wa
Bongo Flava waliobobea kwenye muziki wa live, huwezi kuacha kumtaja Banana
Zorro.
Muimbaji huyo anayetoka kwenye familia
ya muziki – baba yake akiwa Mzee Zahiri Zorro, gwiji wa muziki wa dance, Banana
amejikusanyia weledi na uzoefu mkubwa wa kuimba live kupitia bendi yake, B
Band.
Na sasa akiongea na mtangazaji wa Kings
FM, Prince Ramalove, muimbaji huyo wa Nzela amewataja wasanii wawili wa Bongo
Flava anaowakubali kwa kuimba live. Wasanii aliowataja ni Barnaba na Ruby.
Wawili hao licha ya kuwa na uwezo
katika kuimba muziki jukwaani, kwa sasa wanafanya vizuri redioni na nyimbo zao
‘Lover Boy’ na ‘Walewale’ huku Ruby akidaiwa kufanya maajabu kwenye msimu mpya
wa Coke Studio Africa.
Kwa upande mwingine, Banana amekiri
kuwa muziki wa live unazidi kukua Tanzania, kitu anachosema alikuwa
akikipigania kwa kipindi kirefu.
Dully Sykes, amekuja kivingine na tour ya Dar ‘kwa mara ya kwanza atakuwa
na mabaunsa’
Msanii
wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Inde’ Prince Dully Sykes amejipanga kuja
kivingine katika tour yake jijini Dar es salaam ambayo itaanza weekend hii Club
71.
Akiongea
na Bongo5 Alhamisi hii, Dully amesema ameamua kufanya baadhi ya mabadiliko
kwenye team yake ili kuonyesha utofauti wa Dully wazamani na huyu wa sasa.
“Mikoani
mambo yalikuwa mazuri sana namshukuru Mungu na sasa ni zamu ya Dar es salaam,”
alisema Dully “Tour yangu ya Dar itaanzia Club 71. Kutakuwa na surprise
zakutosha, pia Dully nitakuja kivingine nikiwana na mabaunsa, kwa sababu huyu
pia ni Dully mpya ambaye anahitaji usalama kwenye show zake,”
Muimbaji
huyo amesema katika show hiyo atasindikizwa na wasanii ambao atawaweka wazi
hapo baadae.
Sam wa
Ukweli aitaja Al Jazeera ndiyo walionizima
Msanii wa Bongo Flava aliyetamba na wimbo ‘Sina Raha’ Sam wa Ukweli
amefunguka na kutoa sababu iliyomfanya akae kimya kwa kipindi kirefu.
Muimbaji huyo amesema kuwa lebo yake ya Al Jazeera ndiyo
iliyosababisha awe kimya kwa muda mrefu.
amesema alitaka kuvunja mkataba na lebo ya Al Jazeera kutokana na
kuona hakuna kazi iliyokuwa inafanyika, hivyo alitaka kuwa huru lakini ilishindikana
na aliambiwa alipe shilingi milioni 100 kama anataka kutoka kwenye lebo hiyo,
hali hiyo ilinifanya akae kimya kwa muda mrefu.
Muimbaji huyo ameongeza kuwa mkataba wake na lebo hiyo
umeshamalizika na sasa yupo tayari kufanya kazi na mtu yoyote.
Kala Jeremiah ameleza kwanini mwaka huu
hana mpango wa kuachia albamu
Msanii
wa muziki wa hip hop Kala Jeremiah amefunguka na kusema kuwa mwaka huu hana
mpango wa kuachia albamu mpya kutokana na kazi kubwa ambayo aliifanya katika
albamu yake iliyopita.
Kala
amesema albamu yake iliyopita bado inaendelea kumpatia mshavu mpaka sasa.
amesema
kweli kazi ambayo aliifanya kwenye albamu yake iliyopita ilikuwa ni kubwa sana,
albamu ilikuwa na nyimbo 23,” Hata
msanii afanye vipi hawezi kuachia nyimbo 23 ndani ya mwaka mmoja hata miwili
kama ukiamua kuachia wimbo mmoja mmoja, kwa hiyo yeye anajua bado albamu yangu
ina muda wakutosha kwa wananchi, mwaka huu hana mpango wa kuachia albamu,
Rapa
huyo alisema albamu hiyo bado inaendelea kumpatia mashavu mbalimbali katika
muziki wake kwa kuwa hiyo ni CV ambayo anatembea nayo katika maisha yake ya
muziki.
Kala
kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Wanandoto’ ambao aliutoka miezi miwili
iliyopita.
Msami
ameeleza sababu za kuachana na Irene Uwoya
kama
wewe utakuwa ni mpenzi wa kufuatilia mahusiano ya mastaa basi penzi la Mrembo
kutoka Bongomovie (Irene Uwoya) na Mkali kutoka Bongofleva (Msami)
litakuwa sio kitu kigeni kwenye macho yako sasa leo Msami ameweka
wazi sababu za kuachana na Ireen Uwoya
‘amesema
“kuachana kama
kuachana mimi sioni kama tumeacha kwasababu mimi na Ireen bado tunawasiliana
sema tu mimi niliona kuna vitu haviendi sawa nikaamua kukaa pembeni yaani sina
sababu maalumu ila niliamua tu mwenyewe.”
Maneno ya msami…
Bobby Shmurda aenda miaka saba jela
Baada
ya kukubaliana na upande wa mashtaka, rapper Bobby Shmurda kutoka Brooklyn,
amehukumiwa kwenda jela miaka saba Jumatano hii.
Mwezi
uliopita, Bobby alikiri mashtaka ambayo yaliyokuwa yanamkabili ya kumiliki
silaha kinyume cha sheria. Shmurda aliambia mahakama kuwa alilazimishwa na
mwanasheria wake kukubali hukumu hii ili asihukumiwe miaka mingi zaidi.
Mwanzo
alikuwa amehukumiwa miaka 5 lakini alikuwa hajakubali kwasababu rafiki yake,
Chad “Rowdy Rebel” Marshall alikuwa amehukumiwa miaka 12 kwahiyo ikabidi
aongezewe ili rafiki yake apunguziwe. Wote wamehukumiwa miaka 7 na mahakama.
Jaffarai hataki
kufanya kolabo na mastaa, anataka kuwasaidie wasanii wachanga
Msanii
mkongwe wa muziki, Jaffarai, amesema kuwa hataki kufanya kolabo na mastaa bali
atakuwa anafanya kolabo na wasanii wachanga ili kuibua vipaji vipya.
Rapa
huyo ambaye yupo mbioni kuachia wimbo mpya hivi karibuni, amesema kuwa alikuwa
kimya ili kupisha shughuli za fiesta ambazo zinaendelea.
Kwamba
Kuna kazi mpya inakuja, ni kolabo na msanii na mchanga kabisa, mimi sitaki
kufanya kolabo na mastaa,” alisema Jaffarai.
Aliongeza,yeye
ni msanii mkongwe, kuna namna nyingi ya kuwasaidia wasanii wachanga kwa kufanya
nao kolabo, kwa hiyo yeye anasema mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya
kazi mpya,”
Wimbo
wa mwisho kuachia rapa huyo ulikuwa ni ‘Wakati’ ambao alimshirikisha Kassim
Mganga.
Jennifer Lopez aungana na NBC
kutengeneza series mpya
Kituo
cha runinga cha NBC kimeungana na Jennifer Lopez kutayarisha tamthilia
iliyopewa jina C.R.I.S.P.R.
C.R.I.S.P.R.—
ambayo ni kirefu cha ‘clustered regularly interspaced short palindromic
repeats’ ni tamthilia ya kisayansi.
Hiyo
haitakuwa mara ya kwanza NBC inafanya kazi na Jennifer. Wameshirikiana kwenye
tamthilia Shades of Blue. Lakini pia Lopez atatayarisha na kuwa jaji wa
mashindano ya kucheza ya World of Dance.
Pamoja
na NBC, Lopez ana mradi wa tamthilia ya sheria na CBS huku pia akitarajiwa kucheza
kama muuza unga, Griselda Blanco kwenye filamu ya TV ya HBO.
Bondia Dulla Mbabe kuzipiga na Mchina
Dar 28 Oktoba
Bondia
kutoka Tanzania Dulla Mbabe anatarajia kupanda ulingoni tarehe 28/2016 mwezi
Oktoba, kupambana na Bondia Chengbo Zheng kutoka Taifa la China Pambano la WBO
litafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
Mwandaaji
wa pambano hilo Jay Msangi amesema mshindi wa pambano hilo atajinyakulia Mkanda
wa ubingwa, huku pia kukiwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi ambayo
yatawakutanisha mabondia kutoka Tanzania na nje ya Tanzania.
Jay
Msangi ameongeza kwa sasa wataandaa mapambano mengi ya kimataifa kwa mabondia
wa Tanzania kwa lengo la kuwandaa kufuzu mashindano ya Olimpiki nchini Japan.