Miongoni mwa majukumu ya
mwanaume katika mahusiano ni kuhakikisha anamhudumia mwenza wake ila kuna muda
inakuwa too much yaani mwanaume anakuwa kitegauchumi hata kama hakuna sababu ya
msingi anaombwa hela tu na sio wanawake tu bali kuna na wanaume wanawategemea
sana wake zao na wanawatesa mno wakidai pesa au matumizi.kutokana na hili edonetz
imekuandalia njia za kufata pindi unapoona tabia hiyo imekomaa kwa mpenzi
wako.kama ifuatavyo…
MFUNDISHE KUKUSAIDIA
Wanaume wengi
wanalisahau jambo hili la kutokuwafundisha wapenzi wao, wajibu wa kutoa,
Utakuta kila kitu ananunua yeye, hata nauli ya daladala analipa, wakati
mpenzi wake ana kazi yake, Ifike wakati kwa makusudi, mwanaume ampe
majukumu ya kufanya mpenzi wake, hiyo itamsaidia mwanamke kujua namna pesa
zinavyokuwa hazitoshi na akaweza
kubana matumizi.
kubana matumizi.
KUWA BAHILI
Wapo wanaume tangu wanatongoza wanakuwa ni wafujaji wakubwa wa pesa kwa kutoa ofa na zawadi kibao, Hii inaweza kumjengea imani mpenzi wako kuwa wewe unazo, Wakati akiwa anaamini hivyo, ukweli ulionao moyoni ni kwamba huna fedha za kutosha.

Unachotakiwa kufanya mapema ni kudhibiti matumizi yako hata kama
pesa zinakuwepo, Ifahamike kuwa kutoa hakusababishi uhitaji,
kadiri unavyotoa ndivyo unavyoongeza mahitaji, Weka maisha yako katikati
usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.
usijidai tajiri kumbe ni kapuku tu.
MUWEKE WAZI
Mueleze wazi kuwa huna wakati mpenzi wako anakuomba na kamwe usijaribu kutoa ahadi ambazo huenda ukashindwa kuzitimiza, Usiwe mtu wa kutoa ahadi za uongo, mara nitakununulia hiki na kile. Mwanaume hatakiwi afahamike siku ana pesa au hana. Maana kuna wenzangu ambao siku za mishahara wanabadilisha hadi kutembea Mwanamke akijua hilo naye ataongeza mizinga ili afaidi.

Elewa tu mapenzi si kukomoana, mapenzi ni kusaidiana, Jenga
tabia ya kumsaidia mwenzako ili siku moja na wewe ukiwa na tatizo
akusaidie,Kitu unachotakiwa kukiepuka ni kuwa tegemezi hadi unakuwa
kero, Kumbuka kumpiga ‘mizinga’ mpenzi wako kila mara kunapunguza mapenzi
jiunge nasi
fb@edonetz twiter@edonetz, inst@edonetz_blog na youtube@edone tv