kumbe joto sio kero tu
kwa wanadamu bali hata kwa wadudu kama siafu ambao hushindwa kuhimili joto kali
ambalo hukatisha uhai wao na ndio maana kwa kiasi kikubwa huwezi kuwaona katika
jiji la dare s salaam.
Siafu waishio katika
Jangwa la Sahara husafiri umbali mrefu kutafuta wadudu waliokufa ambao ndio
chakula chao kikuu. Jangwani joto ni kali sana hali inayowafanya siafu hao
kurudi nyumbani kwa kasi ili wasife njiani; lakini swali la msingi hapa ni
siafu hawa wanawezaje kurudi makwao bila kupotea njia?
Utafiti uliofanywa
umethibitisha kuwa siafu wanarekodi hatua zao ili kupima umbali waliosafiri,
ripoti mpya iliyotolewa kwenye tovuti ya Gazeti la Sayansi inaonesha kuwa si
kama tu wanapima umbali kwa kurekodi hatua zao, bali pia kwa macho yao. Njia
yao ya kupima umbali ni kama ambavyo binadamu anavyokadiria kwa macho umbali na
mwelekeo aliokwenda mara awapo kwenye gari.
Watafiti walifunika
macho ya siafu kwa rangi ya njano, ili kujua kama wanaweza kurudi nyumbani au
la bila kuona. Matokeo yanaonesha kuwa, siafu wanaotembea kwa miguu yao
wanaweza kurudi nyumbani bila kuona, lakini siafu wafanyakazi waliokwenda mbali
kwa kubebwa na siafu wengine hawawezi kurudi. Kama macho yao hayajafunikwa,
basi ingawa hawajui siafu waliowabeba walitembea kwa hatua ngapi, bado wanaweza
kurudi nyumbani kwa kupima umbali kwa macho yao. Hili ni jambo la kushangaza,
kwani kabla ya hapo wanasayansi walifikiri macho yao hayawasaidii sana.
Watafiti walisema
mazingira ya siafu hao ni magumu sana, inawabidi kujifunza njia mbili za kupima
umbali, yaani kuhesabu hatua na kuona
jiunge nasi
fb@edonetz, twiter@edonetz, inst@edonetz_blog na youtube@edone tv