Ukiachana na mawifi ndugu jamaa na marafiki mtu pekee ambae
anaweza kujenga au kubomoa ndoa yako na mkwe wako na kama tunavyojua kila mtu
ana staili yake ya maisha kwa hiyo unapoingia katika imaya yake kiukweli
unatakiwa kumsikiliza na kutumia mda kadhaa ili kusoma aina ya maisha
wanayoishi, Maranyingi imekuwa ni tatizo kwa mtu na mkwe wake (hasa mke na mama
mkwe) kuishi kwa umoja na upendo. Utakuta mama anaona ni vigumu kuacha mtoto
wake wa kiume apangiwe mambo yake na mtu mwingine(mkewe) na mke naye anaona
tabu kuchanganyika na familia ya mume. Tatizo hili linaweza kuwa kubwa hata
kuhatarisha ndoa na familia. Uelewano na hekima inahitajika sana kutatua
matatizo haya.
Hapa nimefafanua baadhi ya mambo machache yanayoweza kukusaidia
kuboresha mahusiano yenu.
1.
Onyesha upendo kwa vitendo
Usiruhusu kuongozwa na hisia zako, bali umruhusu Mungu akuongoze
ili uweze kutenda kwa upendo. Haijalishi unajisikia vipi, chagua kutenda
matendo ya upendo kwa mkwe wako (mama au mtoto). Amini kwamba unapoonyesha
upendo Mungu atakufungua moyo wako na kukuwezesha kujisikia vyema.
2. Uwe
mvumilivu
Usiwe na mategemeo makubwa kuwa siku ya kwanza tu kuonana basi
mtapendana na kuwa na mahusiano ya karibu. Jipe mda na pia mpe na yeye muda kwa
kuishi kwa kuvumiliana na hatimaye mahusiano yetu yatakuwa na kuimarika.
usijaribu kumlinganisha na mama/mtoto wako bali umkubali kwa jinsi alivyo. Pia
jaribu kuishi vile ulivyo na usijaribu kuwa mtu mwingine ili kumpendeza mkwe
wako.
3.
Heshima
Wewe kama ni mke hakikisha unamuheshimu mkwe wako kama mzazi
wako na wewe mama kumbuka kuwa mtoto wako ameshakuwa sasa na mkewe ni sehemu
yake hivyo heshimu maamuzi yao na uhuru wao. Usiingilie kila kitu
wanachokifanya bali subiri hadi pale watakapokuomba ushauri.
4.
Tatueni Migogoro
Msiache uchungu na maumivu yakaweka ukuta kati yenu sababu ya
kutokutatuliwa. Kama kuna mmoja amemjeruhi mwingine (mara nyingi huwa ni kwa
bahati mbaya), hakikisheni kuwa mnatatua jambo hilo mapema na kwa upendo.
Uwe tayari kukiri kosa pale unapokuwa umekosea na pia uwe ni mtu wa msamaha.
Kama kuna mmoja anaonyesha hataki kubadilika, muombee na uwe naye kwa akili na
sio kubishana naye.
5. Weka
Mipaka
Lazima kuwe na mpaka ili kila mmoja ajue anatakiwa kufanya nini
na kwa kiasi gani. Muwe mmekubalia jinsi ya kukabili mambo fulani ya kifamilia
na kwa mipaka gani ili asiwepo wa kufanya asivyotakiwa na kuleta kutokuelewana.
6. muonyeshe
urahisi wa kuzungumza na wewe.
Badala ya kuhukumiana kutokana na tofauti zenu, Jishushe na
ufahamu kuwa kuna mengi ya kufundishana kutokana na tamaduni na desturi zenu
mbalimbali. Jitahidi kujifunza toka kwake kadiri inavyowezekana na muombe Mungu
akuwezesha kumkubali jinsi alivyo. Muonyeshe upendo na kumthamini kwa dhati.
Ungana nasi kwa kutufuata kupitia
fb@edonetz, twiter@edonetz, inst@edonetz_blog na
youtube@edone tv