Kutekenya ni jambo lililowapa changamoto wanasayansi wengi. Waliumiza vichwa kujua kwa nini mtu hucheka au kushtuka anapotekenywa.
Wanasayansi wamekuwa wakijiuliza kwa nini watu hucheka wanapotekenywa ilhali tendo hilo ni la mguso?

Ni kwamba kitendo hicho hutokea baada ya ubongo kufanya kazi yake.
Ni kwamba kwenye miili yetu kuna sehemu ya ubongo inayohusisha hisia kama kusikia, kuona, kupiga chafya au kuonja na vitu vyote hivyo hutafsiriwa kwenye ubongo.
Kwa hiyo kunahusisha zaidi ngozi, ndiyo maana mtu akikugusa kidogo unapata hisia za kipekee ambazo zinanaweza kukufanya ucheke au ukasirike
unapotekenywa taarifa hupelekwa kwa haraka hadi kwenye ubongo na kutuma ujumbe kisha ujumbe huo hutafsiriwa na kumpa binadamu taarifa. Hapo ndipo mtu huweza kucheka au kukasirishwa na kitendo hicho.
Wapo wanaostahimili mtekenyo na wengine hawawezi kustahimili. Ndiyo maana wengine hawacheki wakitekenywa au wanatekenywa hawakasiriki, hawacheki lakini wanaruka na kujizuia au kukimbia.
Kadhalika ni kwamba ubongo ni miongoni mwa maeneo magumu katika mwili kuyafafanua na kuelezea utendaji wake kwani hufanya kazi kwa kasi zaidi ya umeme.
Aina za mtekenyo
zinatajwa aina mbili za mazingira ya kutekenywa. Kwanza ni gargalesis huku ni kutekenywa kwa nguvu kunakosababisha kicheko hasa pale unapotekenywa kwapani au tumboni.
Pili ni knismesis ambayo huhusisha mshiko mdogo wa kawaida kwenye maeneo yenye hisia na kusababisha mshtuko mdogo badala ya kicheko.

Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa Kutekenya kunahusisha ubongo kwa sababu
Utafiti wa wanasayansi, wanasema mtu anapotekenywa hucheka kwa sababu ya kujilinda na si kuwa tendo hilo linachekesha.
Kwa kuwa Maeneo yanayotekenywa ni maeneo dhaifu ya mwili kama shingo, tumbo au kwapa, hivyo yanapoguswa mtu hucheka ili kuzuia kitendo kile.
Utafiti wanasema binadamu hujifunza kucheka pindi wanapotekenywa tangu wakiwa watoto wachanga na ili kujilinda na kuwa kicheko hicho ni kielelezo cha kujihami.
Kadhalika wanasayansi wamegundua kuwa baadhi ya watu hucheka hata kabla hawajatekenywa, kwa kutishiwa tu kuwa wanataka kutekenywa.
wanasayansi wa mishipa ya fahamu wanasema kucheka baada ya kutekenywa kunaunda upendo kati ya mzazi na mtoto.
Kama mtu anasema anachukia kutekenywa hana sababu ya msingi, kwani anasahau kuwa njia ya kwanza ya mawasiliano kati yake na mzazi ilianzia hapo.
Kwa nini huwezi kujitekenya na kucheka?
Ingawa wanasayansi wanaeleza kuwa ukitekenywa unacheka, lakini ni vigumu kujitekenya wewe mwenyewe na kucheka.
Inaelezwa kuwa unapopanga kujitekenya, tayari ubongo wako huwa na taarifa hizo, hivyo unajiweka tayari kufahamu kuwa tendo gani linafuata jambo linalozuia kutekenyeka.
Kiuhalisia, tendo la kucheka au kupata hisia zozote baada ya kutekenywa hupungua kwa sababu sehemu ya ubongo inayosababisha kicheko baada ya kutekenywa huwa imepata taarifa.
Katika jarida la saikolojia na, linaeleza kuwa watu hawawezi kujitekenya na kucheka kwa kwa kicheko cha namna hiyo kinahitaji mshtuko unaoundwa na watu wawili kama ilivyo kwa utani.
Lakini jambo hili ni la kisaikolojia pia kwani mtu akiwa na hasira hawezi kucheka hata akitekenywa.
kwa mara nyingi marafiki, ndugu, wenza au watu wa karibu,ndiyo wanatekenyana na kucheka lakini si watu wasiofahamiana.
Ni kwamba kucheka na kutekenywa vina uhusiano kwa kuwa vyote vinahusisha hisia za furaha. pia mtu hawezi kucheka mpaka awe na hisia za furaha au atekenywe na mtu anayemfahamu.
Pia, utafiti unasema watu hutofautiana maeneo ya kutekenywa. Kwa mfano, wengine watacheka wakitekenywa miguuni, wengine shingoni au tumboni.

Baadhi husisimka wanapotekenywa maeneo ya miguuni, lakini hucheka wakitekenywa kwapani.
 
Top