Kitambi
ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na
kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine
kufikia hatua ya kunin’ginia.
AINA
KUU 6 ZA VITAMBI.
kinapatikana kwa kula sana kitimoto
2. KITAMBI MCHUCHUMIO - Hiki
kitambi kimekaa kama herufi D kinatokana na kula sana michemsho na bia za ofa
3. KITAMBI
MBONYEO - Akivua shati kitovu hakionekani. Hiki wanacho wala rushwa,
ila akisimamishwa kazi kinaisha haraka sana.
4. KITAMBI
MTEPETO - Ni kitambi cha wastani ambacho ukivaa nguo pana
hakionekani. Hiki kinasababishwa na kula mno vipolo
5.
KITAMBI MFUMANIO - Hiki mtu anakuwa hana pesa ila kitambi ni
kutokana na minyoo na utapiamlo wa ukubwani
6. KITAMBI
MTUNGUO - Hiki wanacho sana akina dada na wanawake, kina umbo la
yai. Hiki kwa "diet" hakitoki labda kwa maombi tu. Share na washikaji
zako.
JINSI
KITAMBI KINAVYO PATIKANA
Kwa mujibu wa
tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli
kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika
sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
Kwa wanawake seli hizo
zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye
makalio.
Kwa upande wa wanaume
seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio
pia.
Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi
hukusanywa kwa njia kuu mbili:
i. Njia ya kwanza
ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
ii. Na njia
ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k
SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni
kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa
mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula
vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama
taka mwili.
Vyakula vinavyochangia kuleta
kitambi ni pamoja na
:
i. Vyakula vyenye
mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa
kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama
kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa
yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi,
na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.
ii. Vyakula vyenye wanga mwingi
kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.
iii. Vyakula
na vinywaji vyenye sukari nyingi iliyo
ongezwa
kama vile soda
na keki.
iv. Vyakula vilivyo
tengenezwa kwa ngano na sukari kama vile
keki, skonzi, chapatti, maandazi, mkate mweupe nk
v. Pamoja na
vinywaji vilivyo tengenezwa kwa kutumia ngano
kama vile bia za aina mbalimbali na nk
Vyakula vilivyo
tajwa hapo juu, vikitumiwa bila kuzingatia
kanuni za mlo kamili, huchangia kuleta
tatizo la kitambi.
vi.Sababu nyingine ni
kutofanya mazoezi ya mwili na viungo
kwa muda mrefu.
JINSI YA KUJUA KAMA UNA KITAMBI
Kitambi kinaweza kuonekana kirahisi
kwa macho. Ila kujua ni kwa kiwango gani kitambi chako kipo inabidi kufanya
vipimo vya kiuno na nyonga
Mzingo wa kiuno ukiwa >102 cm au
40 kwa wanaume na >88 cm au 35 kwa wanawake, na uwiano wa kiuno
na hips(Waist-Hip Ratio) ikiwa >0.9 kwa wanaume na >0.85 kwa wanawake.
BMI ya 30 au zaidi inaashiria ‘Obese’ uzito kuzidi kiasi. Kuwa
na mzingo uliozidi kawaida ni kiashiria hatari cha matatizo ya kimetaboliki,
kuliko hata cha BMI.
Kipimo kingine cha kitambi ambacho
kimeonyesha uwezo zaidi kuliko BMI katika kutabiri uwezekano mkubwa wa magonjwa
ya moyo ni Index Of Central Obesity(Waist-To-Height
Ratio-WHtR) ambapo uwiano ukiwa sawa na 0.5 au zaidi, hii ikimaanisha
mzingo wa kiuno angalau ni nusu ya kimo cha mtu.
Kipimo kingine ni Body Volume Index,
kinachopima kitambi kwa kupima umbo la mtu na mgawanyo wa uzito wake.
MAMBO YANAYO MUWEKA
MTU KATIKA HATARI YA KUPATWA NA KITAMBI
Tumekwisha ona
hapo juu jinsi kitambi kinavyo patikana na
vyakula pamoja na sababu nyinginezo zinazo
sababisha kutokea kwa kitambi, sasa tutazame
mambo yatakayo kufanya uwe katika hatari
ya kupatwa na kitambi.
Kwa mujibu wa
tafiti mbalimbali za kitaalamu, mambo yafuatayo
huwaweka watu katika hatari kubwa ya
kupatwa na kitambi :
1.Ulaji mbovu wa chakula; Ulaji
mbovu wa chakula ni ulaji
usio zingatia kanuni za mlo kamili. Hapa
mtu hufululiza kutumia chakula cha aina
fulani pekee bila kuzingatia aina
nyinginezo za chakula. Mfano;
mtu anaweza kuwa anakula mlo ufuatao :
Asubuhi :
Mchemsho ama supu ya ng’ombe ,
chapatti tatu na soda moja. Mchana : Ugali nyama choma
anashushia kwa maji na soda.
Jioni
: Mchemsho wa kuku na bia
mbili nakuendelea.
Usiku
: Chips mayai au chips kuku
au chips mishikaki na bia.
Mtu
huyu akiendelea na utaratibu huu kwa
muda mrefu, ni lazima atapatwa na kitambi.
2. Ulaji mfululizo
wa vyakula vyenye mafuta mengi
3. Ulaji
mfululizo wa vyakula vyenye wanga mwingi .
4. Ulaji mfululizo
wa vyakula vyenye sukari iliyo ongezwa
5. Ulaji mfululizo
wa vyakula vya ngano.
6. Ulaji mfululizo
wa vinywaji vyenye ngano na sukari.
7. Kutofanya mazoezi
ya mwili na viungo
Mhusika anapokuwa
katika makundi yote yali yotajwa hapo juu,
hali huwa mbaya zaidi.
NJIA ZA KUONDOA KITAMBI
Kuwa na kitambi
ni lugha ya mwili ( body-language ) inayo
leta ujumbe kwako kwamba “ Mwili wako haupo salama tena “
Kama una
kitambi maana yake una mafuta yasiyo
hitajika mwilini, mwili wako unatumika kuhifadhi
mafuta usiyo yahitaji.
Hali hii kitabibu
imaanisha kwamba, ogani nyinginezo zilizomo ndani
ya mwili wako zinao gelea kwenye mafuta yasihotajika
yaliyomo ndani ya mwili wako, jambo linalo
kuweka katika hatari kubwa sana
ya kushambuliwa na magonjwa hatari kama
vile shinikizo kubwa
la damu, kiharusi na kisukari na kwa kutaja
machache.
Hivyo basi ili
kuondokana na hatari hiyo, yakupasa
kupambana kuondoa hayo mafuta yasiyo
hitajika mwilini mwako.
NJIA ZA KUONDOA
KITAMBI.
Unaweza kuondokana
na kitambi kwa kufanya diet pamoja na
mazoezi ya mwili na viungo.
Vilevile unaweza
kuondoa kitambi na kupunguza mafuta mwilini
kwa kutumia dawa asilia ya kuondoa
kitambi na kuondoa mafuta yasiyo hitajika
mwilini.
Mi naona sanasana ni vizuri kufanya
mazoezi ili kuondokana na kitambi au kupata ushauri wa dakitari moja kwa moja