Mafua ni ugonjwa ambao chanzo chake ni kuathirika kwa mirija ya kichwani ya mfumowa kuvuta pumzi. Athari hizo huletwa na virusi vya aina mbalimbali kupitia kwenye hewa au mavumbi na ni ugonjwa unaoambukizwa kwa haraka sana.
Miongoni mwa dalili za mafua ni pamoja na kuumwa kichwa na homa kidogo, kikohozi au kukereketwa kohoni, kuchuruzika kwa kamasi (aina ya majimaji) puani pamoja na uchovu na maumivu ya maungo.
Na Orodha ya vyakula vifuatavyo vimeelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha  kinga ya mwili na kupambana na  maambukizi mengine kwa kuwa na kiasi  kikubwa cha protini na virutubisho vingine.
SUPU YA KUKU
Supu ya kuku wa kienyeji inaelezwa kuwa  na virutubisho vinavyosaidia kupunguza  utokaji wa mafua.
Utapata virutubisho vingi zaidi  ukitengeneza supu ya kuku kwa  kuchanganya na mboga za majani. Weka chumvi kiasi kidogo katika supu hiyo.
VITUNGUU  SAUMU
Vitunguu saumu vina kirutubisho aina ya  ‘allicin’ ambacho kina uwezo wa kutoa  kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ya  kuambukiza.
Kitunguu saumu kinatoa kinga hali kadhalika kinapunguza muda wa mtu  kuumwa na mafua.
Tumia kitunguu hicho kwa kupika kwenye  chakula au kwa kutafuna punje zake.

MACHUNGWA, PILIPILI KALI
Utafiti unaonesha kwamba, ulaji wa vyakula  vyenye Vitamin C kwa wingi kila siku  husaidia kuondoa au kuzuia ugonjwa wa  mafua.
Machungwa ni miongoni mwa vyakula  vyenye kiwango kikubwa cha Vitamin C. Pamoja na machungwa, mboga za majani  aina ya Brokoli na pilipili kali.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top