Ni vizuri ukajua mambo haya niliyo kuwekea ambayo unatakiwa
kufanya Baada ya kuoga, usiharakishe kutoka bafuni, kwanza kagua mwili wako
mbele ya kioo, ukikagua kwa makini, pengine unaweza kugundua matatizo kadhaa ya
afya na ikakusaidia sana kigundua tatizo na kulisuruhisha .
1. Kwanza angalia nyusi zako, kama nyusi zako zinabadilika na kuwa
nyembamba zaidi au kuwa fupi zaidi kila siku, basi uchukue tahadhari katika
tezi zako.
2. Kagua mdomo na meno yako, kama ulimi wako umefifia, basi
pengine damu imepungua mwilini na ukiwa na madoa meupe kwenye meno yako, usiwe
na wasiwasi, hii ni kutokana na kutumia dawa za meno zenye floridi mara kwa
mara.
3. Halafu macho yako, ukiona macho yako yana madoa ya manjano,
basi uwe na tahadhari na ugonjwa wa ini;
4. Na kama wewe ni mwanamke, ukigundua nywele zako zimepungua
sana, lakini nywele katika sehemu nyingine kama tumbo na miguu zimeongezeka
sana, basi utahadhari na ugonjwa wa ovari na bora uende hospitali kuangaliwa na
daktari.
5. Kagua miguu yako, mishipa yako ya damu ikiwa na rangi ya
zabibu na kujitokeza waziwazi na ukiona inauma, basi bora uende kwa daktari,
kwani pengine umepata ugonjwa fulani wa mishipa ya damu
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv